Waziri Gwajima awatupia mzigo bodi ya Sanaa kuhusu maudhui ya Msanii Willy Nass anayetaka Penzi na mama yake

Waziri Gwajima awatupia mzigo bodi ya Sanaa kuhusu maudhui ya Msanii Willy Nass anayetaka Penzi na mama yake

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Kutoka kwa Wananchi waliokerwa na kunitumia taarifa hii;

Huku online kurasa mbalimbali, anayedaiwa kuwa ni Willy Nass na anayejulikana kama msanii wa comedy na content creator wa mitandaoni, ameandaa na kusambaza comedy ya ajabu inayohusu eti mama na mtoto wake kuanzisha uhusiano wa mapenzi. Sijui kama msanii huyu ana usajili wa bodi ya filamu au anafanya kazi bila usajili.

Taarifa zinaonesha anatumia Facebook followers 42,000
Instagram 4,000
Tiktok 5,3490.
You tube 1,200.

Aidha, Wananchi wanasema, content zake zote anazotengeneza kwenye kurasa zake zina maudhui yanayofanana kwamba, zina udhalilishaji hasa kwa wanawake huku akifanya content zote hizo kwa series (episodes).

Sasa, watazamaji wa kurasa hizo, kila mmoja anashangaa na wananitumia mimi @gwajimad kunitaka nichukue hatua ambazo kimsingi udhibiti wa kazi hizi ni Mamlaka ya Bodi ya Filamu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (nimeshawapa taarifa) kwa hatua zaidi.

Hivyo, ndugu Wananchi, kwa watu aina hii, tuwe tunatoa taarifa mamlaka husika ili, wafahamu, wachukue hatua stahiki za kulinda maadili yetu kwani, mambo aina hii yana promote mmomonyoko wa maadili.

Nitaleta baadae elimu ya vyombo mbalimbali vya mnyororo wa udhibiti wa maadili ya jamii kwa ujumla na jamii zake mbalimbali kwa mujibu wa Mwongozo wa Maadili ya Taifa ili, mfahamu na muwe mnatoa ushirikiano mahali sahihi kwa wakati sahihi.

Ndugu Wananchi, Ahsanteni kwa ushirikiano.

Bodi Ya Filamu Tanzania
@tanzania_film_board @basata.tanzania @wizara_sanaatz @prof.kabudipjam @gersonmsigwa
@chuma_kaole @maendeleoyajamii
 
Mdau akamtaka aingilie pia Ishu ya anko T

Screenshot_20250914-095106.png
 
Kuna mjuba mmoja yeye aliimba nakupenda bibi kizee, nakupenda kikongwe. Tulijiuliza kama huyo mjuba ana adabu au hana kwa nini atake penzi la mtu mzima anayemuita mjukuu!
 
Tanznia kuna wasanii wengi sana wajinga wajinga na hao ndio role models wa vijana wa kileo.
 
Back
Top Bottom