The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Kufuatia kufunguliwa kwa shule, waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu amekemea vikali tabia ya BAADHI ya Wazazi na BAADHI ya Walimu kupiga watoto kupita kiasi BILA KUFUATA KANUNI ZA UTOAJI WA ADHABU STAHIKI.
Amesema adhabu za kupitiliza zinawajengea watoto hali ya woga, zinaharibu uwezo wao wa kujieleza, na mara nyingine zinaweza kuwanyima msaada muhimu pale wanapokabiliwa na changamoto. ameendelea kwa kusisitiza umuhimu wa kutumia njia za mazungumzo na urafiki katika kumrekebisha mtoto badala ya kutumia fimbo mara kwa mara.
“Mfanye mtoto awe rafiki yako, awe huru kukueleza changamoto zake. Kumpiga fimbo kila mara si suluhisho la kumrekebisha zaidi ya kuingia kwenye MGOGORO na SHERIA ya Mtoto . Wazazi wanaoamini kuwa, kupiga watoto ni njia pekee ya kuwafundisha waache Imani na tabia hiyo, kwani si msaada kwa maendeleo ya mtoto. Malezi bora yanahitaji upendo, mazungumzo, na njia shirikishi za kufundisha maadili"