#COVID19 Waziri Gwajima: Kauli ya Hayati Magufuli kuhusu Chanjo inapotoshwa

#COVID19 Waziri Gwajima: Kauli ya Hayati Magufuli kuhusu Chanjo inapotoshwa

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima amesema kauli ya hayati Dk John Magufuli kuhusu chanjo inapotoshwa kwani hakusema watu wasichanje ila kuwe na umakini kutokimbilia chanjo bila kujiridhisha.

Waziri Gwajima ameyasema hayo leo Jumatano Julai 29, 2021 wakati wa hafla ya uzinduzi wa chanjo ya Covid-19 inayofanywa na Rais Samia Suluh Hassan, Ikulu Dar es Salaam.

Akimnukuu hayati Magufuli alivyosema, Waziri huyo amesema ilikuwa Januari 27, 2021 wilayani Chato, ambapo Magufuli alisema Wizara ya Afya isiwe inakimbiliakimbilia machanjo bila yenyewe kujidhihirisha.

“Hiki ndicho alichokisema haya Magufuli, wametokea sasa wataalam wakuhariri hii hotuba na kujikita kwenye hicho kivuli na kupotosha.

“Halafu wametokea wasikilizaji wanaosikiliza hicho kitu kikishapelekwa wanaenda nacho kuwapotosha wengine, ndugu zangu Watanzania hili jambo sio zuri, ndugu zangu wanahabari hili jambo sio zuri, hotuba za viongozi ni za kuziheshimu ni za kuzichukua kama zilivyo ziende, wananchi waamue wenyewe.

“Kwa hiyo leo nakemea upotoshaji huu unaofanywa na nikushukuru Rais kwa kusimama bila kutetereka bila kukatishwa tamaa kuiendeleza kazi hii na kutufikisha hapa siku ya leo,”amesema Waziri Gwajima.


My Take:
Tuna viongozi wawili tu wanaitwa Gwajima na wanatuahamishia mada balaa, Tungepata watano sijui ingekuwaje !
 
Aache uongo


FB_IMG_16259397485796455.jpg
 
Kauli ya Magufuli juu ya chanjo
 
Back
Top Bottom