#COVID19 Waziri Gwajima: Maambukizi ya COVID-19 yapo, wasiochukua tahadhari waitikie wito

#COVID19 Waziri Gwajima: Maambukizi ya COVID-19 yapo, wasiochukua tahadhari waitikie wito

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa maelekezo kila mtu avae barakoa kwenye mikusanyiko, hivyo watu wachukue tahadhari.

“Kasi ya wagonjwa kuendelea kujitokeza na kulazwa kwenye hospitali zetu inaashiria maambukizi yapo, watu wasidhani kwamba tunasubiri mpaka iwe mtaani tunaona maiti ndiyo tuanze kazi, kazi inayofanyika ni kuhakikisha hali haiwi mbaya.

“Serikali inajitahidi na Rais amekuwa akikumbusha jamani ndugu zangu tuchukue tahadhari na kujikinga na corona,” amesema Dk Gwajima.

Alitahadharisha kuwa kutokana na kinga ambazo Watanzania wanazo, wasiache kujikinga kwa kuwa wagonjwa wapo na wanaendelea kujitokeza.

“Tunaomba wale ambao hawaitikii tahadhari basi waitikie ili tuongeze wigo ili hali izidi kuwa salama zaidi tusipate idadi kubwa ya wagonjwa, kwenye msongamano vaa barakoa, inawezekana umepona huumwi umebeba unavisambaza, waokoe wengine, kuna wazee na wengine wanaumwa, tukivaa wengi hizi barakoa tunawaokoa wasiovaa,” amesema Waziri Gwajima.

Chanzo: Mwananchi
 
Toeni takwimu za idadi ya wagonjwa walio mahospitali na wanaopoteza maisha, Kwani kuna haja gani ya usiri? Kwani corona ni gono au kaswende?

Hopeless Minister.
 
Toeni takwimu za idadi ya wagonjwa walio mahospitali na wanaopoteza maisha, Kwani kuna haja gani ya usiri? Kwani corona ni gono au kaswende??
Hopeless Minister.
Mlishaambiwa wakitangaza watu watapata hofu, hofu inasababisha upungufu wa kinga mwilini, sio maneno yangu aliyasema Dr. Molel, Naibu waziri wa Afya.

IMG_20210710_112823.jpg
 
Ujanjaujanja
😃😂😁😄😘😅😂😁
Mwafa!!
 
Sijui kwanini serikali isiwatake wananchi wajinunulie mitungi yao ya oxygen ili kujiandaa, watufundishe na jinsi ya kuitumia kwenye TV.
 
Back
Top Bottom