Waziri Gwajima, sikia kilio cha Watoto wanaofanyiwa ukatili, Ubakaji, mimba, ndoa za Utotoni Uyui (Tabora)

Waziri Gwajima, sikia kilio cha Watoto wanaofanyiwa ukatili, Ubakaji, mimba, ndoa za Utotoni Uyui (Tabora)

Torra Siabba

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
243
Reaction score
287
“Nilimkuta binti yangu chumbani kwa mpangaji mwenzangu, mbaya zaidi baada ya upekuzi yule mpangaji kumbe alishamnunulia simu binti yangu, na akampa ufunguo wa chumba ili muda wote akimtaka aweze kuingia kwa ajili ya kufanya mapenzi wakati yeye bado ni mwanafunzi.”

Ni sehemu ya simulizi ya Eliakim Zakayo (sio jina lake halisi) Mkazi wa Kaliua, Tabora akisimulia namna binti yake alivyoingia kwenye mahusiano na mpangaji mwenzake wanayeishi nyumba moja.

Wanajamii Forums naomba nibadilishane na ninyi mawazo kuhusu hii kadhia ambayo imekuwa ikileta sintofahamu huku Tabora.
Uyui Ofisi.jpg
Inawezekana ni takwimu official au la lakini Tabora inajulikana kwa kuwa kinara wa ndoa za utotoni na wilaya inayotajwa kuwa kinara ni Uyui.

Kuna Wazazi wenye tamaa wanaozesha Watoto wao kwa mahali ya ng’ombe, hali hiyo imekuwa ikiwaumiza kimwili na kisaikolojia Watoto wengi wanaokosa haki yao ya kupata elimu.

Mfano huyo mpangaji niliyeanza kumtaja juu alifikisha suala hilo Polisi, mtuhumiwa akakamatwa na kuwekwa ndani, wakati taratibu nyingine zikiendelea katika mazingira ‘tata’ mtuhumiwa akatoka Polisi na kuendelea kutamba mtaani.

Nimezungumza mara kadhaa na baba wa Binti ambapo amefikia hatua anatamani ‘ammalize’ kienyeji kwa sababu anaona Polisi hakuna haki.

Baadhi ya Askari Polisi ni changamoto
Kuna mazingira ya baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi ikiwemo wa Kituo kikubwa cha Polisi Mkoa wa Tabora kushirikiana na watuhumiwa wa kesi kama hizo ili kuzizima chini kwa chini, hali hiyo inachangia ukatili huo kuendelea kufanyika kwenye Jamii.

Eneo la Bukumbi
Bukumbi ni Kata inayopatikana, Wilaya ya Uyui iko mpakani na Kahama na Wilaya ya Uyui yenyewe, idadi ya Wasichana wadogo wanaoozeshwa ni kubwa, hata inapotokea Polisi wanapigiwa simu kujulishwa kuhusu hali hiyo hawajali.

Moja ya changamoto iliyopo ni kuwa Wakazi wengi wa Wilaya hiyo wana mali na wapo vizuri kiuchumi, wanachofanya ni kutumia fursa hiyo kutembeza fedha kwa Maafisa walio waaminifu na hivyo ndoa za utotoni ni nyingi.

Watoto wanaathirika Kisaikolojia, wanabebeshwa mimba wakiwa hawapo tayari kimwili na kiakili, wanakosa elimu, wanakosa haki yao ya kucheza na kufurahia Maisha ya utoto.
Tabora-Uyui.svg.png
Matukio ya ubakaji
Mbali na hali hiyo kuna matukio ya ubakaji ambayo nayo yanapofikishwa kwenye mamlaka ni kama kuna ukimya, Jamii nayo ni kama imekuwa na uoga wa kupigania hali hiyo.

Mbali na hapo kwa Tanzania nzima, takwimu za Jeshi la Polisi zinaonesha kumekuwa na ongezeko la kesi za ulawiti kwa Mwaka 2020, kwa mujibu wa kesi zilizoripotiwa ni 1,205 na ongezeko la mara mbili mwaka 2023 hadi kufikia matukio 2,488 ambalo ni asilimia 57 kulinganishwa na Mwaka 2022.

Changamoto ya kukatisha masomo
Nirejee kwa sasa hali ilivyo, utafiti wangu umebaini kuwa Wilayani Uyui kuna changamoto ya Wanafunzi wengi wa kike wanaoshindwa kuendelea na masomo ya Sekondari (form one na Kidato cha tano) kutokana na mazingira magumu wanayokutana nayo.

Wanafunzi hawana sauti
Nimezungumza na baadhi ya Wanafunzi wa Madaha Sekondari pamoja na Uyui Sekondari Wilayani Uyui wameeleza hisia zao kuwa wanaponzwa na Wazazi na walezi wao kutaka mali, wanaomba Serikali ifuatilie na ichukue hatua dhidi ya wanaohusika wote

Wataalamu wa Afya wao wanasemaje?
Daktari mmoja wa Zahanati ya Ishimulwa, Kata ya Bukumbi ambaye jina lake nalihifadhi, anasema suala la Msichana mwenye umri wa miaka 17 au 18 kuwa na mtoto zaidi ya mmoja ni kawaida huko, lakini kiafya ni mbaya kwa kuwa msichana anapopata ujauzito akiwa na umri mdogo kuna madhara yake kiafya.

Anasema uwezekano wa kupata kifafa cha mimba, mama au mtoto anayezaliwa kuwa hatarini kupoteza maidha kutokana na via vya uzazi kutokuwa vimekomaa.

Daktari anasema mara nyingi wanapokuwa na changamoto ya uzazi ya msichana mdogo wamekuwa wakiwapa rufaa kwenda Hospitali ya Mkoa wa Tabora Kitete au kwenda Kahama Mkoani Shinyanga

Daktari anashauri Ustawi wa Jamii unapaswa kuwepo kuanzia ngazi za Vijiji ili kuokoa kizazi kinachoangamia kwani kwa sasa kwenye Kata ya Bukumbi hakuna Ofisi za Watu wa Ustawi wa Jamii.
Picha ya Mtandao.jpg
Walimu wapo Mahabusu
Hadi sasa naandika andiko hili kuna Waalimu sita wa shule tofauti tofauti wako mahabusu kwa makosa ya kuwalawiti Watoto wadogo katima shule za binafsi.

Makamu Rais alitoa tamko
Kutokana na kuonekana kwamba vitendo vya unyanyasaji wa kingono kwa Watoto, ndoa za utotoni, matukio ya ubakaji ulawiti ilimlazimu hata makamu wa Rais Phillip Mpango kuwaagiza viongozi wa mkoa huo kusimamia maadili.

Dkt. Mpango aliyaeleza mambo ya unyanyasaji kwa Watoto na ndoa za utotoni wakati wa ziara yake aliyoifanya Tabora kuanzia Oktoba 9 hadi 11, 2024, na aliyazungumza kwa nyakati tofauti akiwa kwenye ziara yake hiyo ya kikazi.

RAIS SAMIA AKIWA MAKAMU RAIS ALIELEZA KUUZUNISHWA NA KASI YA MIMBA ZA UTOTONI TABORA
Februari 25, 2019, Samia Suluhu Hassan akiwa Makamu wa Rais alielezea kushtushwa na idadi ya watoto wa kike wanaopata mimba mkoani Tabora na kuagiza hatua za kuia tatizo zichukuliwe.

Alisema idadi ya mimba za utotoni imeongezeka kutoka 21,889 Mwaka 2017 hadi mimba 27,390 Mwaka 2018. Alisema kasi ya uwepo wa mimba za utotoni ni kubwa na haikubali na kutaka viongozi Tabora kubadilisha hali hiyo na kuwataka wazazi wajitahidi kuwalinda watoto wao.
Samia.jpg
Alisema kasi ya uwepo wa mimba za utotoni ni kubwa na haikubali na kutaka viongozi Tabora kubadilisha hali hiyo na kuwataka wazazi wajitahidi kuwalinda watoto wao.

Makamu wa Rais alieleza kuwa wakati mwingine wazazi hawajitokezi kutoa ushahidi pale inapojulikana watoto wao wamepata ujauzito na kwamba na kuongeza kuwa vitendo hivyo ni kuwakatili maisha yao. Alisema kuwa hatua za makusudi zisipochukuliwa kuna uwezekano wa kuwa na wataalamu wa kike wachache kwa sababu ya kushindwa kutimiza ndoto zao.

Soma Pia: Nguvu ya Mabadiliko: Vita Dhidi ya Ndoa za Utotoni katika kijiji cha Twa Twa Twa

Hivyo sasa tunamuomba Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wanawake na wenye mahitaji maalum Mhe. Dkt Dorothy O. Gwajima kuingilia kati katika kusaidia watoto hawa ambao sauti zao hazisikiki kwa mamlaka husika.

SHERIA YA NDOA
Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 inaruhusu mvulana kuoa kuanzia umri wa Miaka 18, na Msichana kuolewa kuanzia Miaka 14 na Miaka 15 kwa kibali cha Wazazi, inamnyima Mtoto wa kike haki zake za msingi hasa Haki ya kupata Elimu.

Serikali imekuwa ikipambana kubadilisha Sheria hii lakini ni kama nayo inaogopa kufanya maamuzi kwa sababu za Kidini, binafsi naona uwepo wa Sheria hiyo ni sehemu ya kuhalalisha ndoa za utotoni.
 
Back
Top Bottom