#COVID19 Waziri Gwajima: Tanzania maambukizi yafikia watu 47 toka 14 kwa siku

Mkuu hebu fafanua kauli nzito sna hii
Hawezi kusema uongo ambao hata zombie atashituka.
Yaani Kati ya Watanzania 10 wanaokufa na Corona 7 hawajachanjwa.
Kwa mahesabu ya darasa la pili waliochanjwa hawafiki 1.5m ya Watanzania 60m.
Maiti zingeokotwa barabarani maana wangekuwa wanakufa Watu wengi Sana.
 
Daaah aise
 
Daaah aise
Halafu wale waliochanjwa wanakufa kwa magonjwa nyemelezi siyo Corona.

Hata walitengeneza chanjo hawawezi kuukubali uongo huu.

Wala hagusii Omicron inayoua hata waliochomwa booster dose.
Mhuni huyu mama.
 
Halafu wale waliochanjwa wanakufa kwa magonjwa nyemelezi siyo Corona.

Hata walitengeneza chanjo hawawezi kuukubali uongo huu.

Wala hagusii Omicron inayoua hata waliochomwa booster dose.
Mhuni huyu mama.
Mama amejibu kitaalamu wewe unakuja na maneno ya korosho tu,
 
Gwajima anafanya kazi nzuri sana aise
 

Hakuna anaeweza kukujibu mkuu! Maana wanapita kimya kimy
 
Atupe maelekezo tuliochanja J and J tunaweza kuchanjwa Moderna au Pfizer naona Israel wanachanja mpaka chanjo ya 4 wengine sio wafuasi wa tapeli Askofu Gwajima
 
Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu kinachotembea.
Your browser is not able to display this video.
Your browser is not able to display this video.
Your browser is not able to display this video.
 
Mkuu Waziri alisema kati ya WAGONJWA kumi waliolazwa, saba hawajachanjwa.
 
Japo siyo mtaalam wa afya ila ninajitahidi kusoma na kuuelewa huu ugonjwa. Ngoja nikushirikishe nilichoelewa:

1. Corona ni aina ya ugonjwa unaosababishwa na kirusi. Kirusi hiki (kama kawaida ya virusi) huendelea kuishi kwa kujibadilisha ili kikabiliane na kinga ya mwili. Kinga ikiwa imara mtu anaweza akapambana nao na kukishinda nguvu kirusi. Sasa wakati wa mapambano kirusi kinauwezo wa kujibadilisha na unapomuambukiza mtu mwingine, unakuta kile kirusi kinaenda kwake na nguvu nyingine. Ndio maana baada ya muda kunakuwa na aina mbalimbali ya kirusi kile kikiwa na mabadiliko ya nguvu na mashambulizi. Sasa hivi ukiugua inategemea umeambukizwa kirusi kipi. Inawezekana ni Omicron au Delta au hata ukute kilishabadilika tena. Mpaka maabara wafanye utafiti wa kirusi ulichonacho ndio wajue ni aina gani.

2. Sifahamu ni variants gani zipo wapi kwa sasa ila Omicron imepewa uzito kwasababu ndio aina mpya iliyozaliwa hivi karibuni. Kuna uwezekano mkubwa sana kwamba zile variant/aina nyingine bado zipo. Kama umechanjwa kinga yako imeongezewa uwezo wa kupambana nao. Yaani virusi havitakudhuru sana kama mtu asiye na kinga yakutosha. Ndio maana wanasisitiza wenye magonjwa nyemelezi au wenye kinga hafifu wachanje. Sasa, tatizo linakuja pale ambapo kirusi kinapoendelea kuambukizana hata kwa watu wenye chanjo kinazidi kujizatiti na mwisho kinajifunza jinsi ya kupambana na kinga za mwili. Kinapozaliwa kingine kinakuwa na uwezo zaidi wa kupambana na kinga hata ile iliyoongezewa kwenye chanjo. Ndio maana wanazungumzia booster shot, yaani chanjo inaimarishwa kudhibiti aina mpya zinazozaliwa. Sasa kirusi chochote tabia yake nikuongezeka kwa kasi, kujizatiti na kusambaa kwa kasi. Ndio maana watu wanatakiwa wachanje kwa wingi ili kupunguza kasi za maambukizi na kusambaa kwa kirusi ili kisipate nafasi ya kujibadili kwa haraka. Chanjo inapunguza kasi ya kusambaza na kuugua sana.

3. Unapo pata chanjo ni kwaajili ya kuuongezea mwili kinga ya kupambana na kirusi pindi ukikipata, pamoja na kupunguza kasi ya maambukizi. Ndio maana unashauriwa kupima kwanza kabla ya kuchoma chanjo. Kama ukikutwa na kirusi cha korona, wanashauri upone kwanza ndio uchome. Kama umeshapata corona na ukapona, mwili hubaki na kumbukumbu ya kinga mpaka miezi mitatu. Yaani ukiambukizwa tena ndani ya miezi mitatu, kinga itakumbuka jinsi ya kukabiliana na kirusi hicho. Chanjo nyingi hukaa hadi miezi sita (kwa taarifa za hivi karibuni), ndio maana nyingine unachoma mara mbili na sasa kuna ya tatu. Kila unapochomwa, chanjo huwa inaboreshwa kukabiliana na aina mpya zinzoibuka. Changamoto ni kwamba, wanasayansi wanaona mabadiliko makubwa kwa kipindi kifupi tofauti na aina nyingine na virusi kama influenza. Kwa wenzetu ambao wanaishi kwenye baridi kali huwa wanachoma booster za chanjo ya influenza kila mwaka, hasa kwa wazee na wenye magonjwa ya kupunguza kinga ya mwili.

Natumaini maswali yako yamejibika. Wataalam wanaweza kuja kuongezea au kukosoa.
 
Corona ni futa, ukijifukizisha katika 100 digrii sentigredi linapasuka paaah, unapona sasa mnaogopa nini ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…