Waziri Hamad Masauni, IGP Wambura leo nitawapa mifano uonevu wa askari wa kituo cha polisi Bunda. Mkifanyie uchunguzi pia chunguzeni haya ninayoyasema

Waziri Hamad Masauni, IGP Wambura leo nitawapa mifano uonevu wa askari wa kituo cha polisi Bunda. Mkifanyie uchunguzi pia chunguzeni haya ninayoyasema

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2023
Posts
445
Reaction score
1,094
Binafsi naiheshimu sana serikali pamoja na viongozi wake kuanzia ngazi za chini mpaka kule juu.Serikali za mitaa zinafanya vizuri pamoja na kuwepo kwa changamoto kadha wa kadha. Hali kadhalika serikali kuu inafanya vyema, changamoto zipo tu hata mataifa yaliyoendelea wana changamoto lukuki tu. Huwa haziishi siku moja. Kikubwa wananchi tuiunge mkono serikali yetu

Tatizo naloliona ni kwa baadhi ya watumishi wa jeshi la polisi hawa ndio wanafanya serikali irushiwe lawama hata kwa mambo yanayofanywa na askari wake kwa utashi wake.Nitatoa mifano hapa Kwa kulenga baadhi ya matukio yaliyowahi kufanya na polisi wilayani bunda.

Mwaka Jana askari mmoja ajulikanae Kwa jina la Juma mzanzibar alikamata kichaa mmoja (maarufu kwa jina la msukule)Askari huyo inavyoonekana alikuwa na uhasama na kijana mmoja ambaye ni mtumishi wa umma.Alichokifanya Askari huyo ni kumbeba kichaa huyo mpaka dukani kwa mtumishi huyo ambapo baada ya kufika aliomba tv iliyokuwa dukani kwa mtumishi huyo (Hitachi matoleo ya nyuma)itolewe ipelekwe kituoni au mtumishi aonyeshe risti ya TV hiyo.

Mashuhuda waliokuwepo wakamweleza askari tv husika Ipo dukani zaidi ya miaka nane.Askari husika hakuwasikiliza badala yake akaita karandinga la polisi ambapo tv iliwekwa tayari kupelekwa kituoni.

Hoja ya askari ni kwamba TV husika iliuzwa kwa mtumishi huyo na kichaa siku mbili zilizopita.Askari huyo hakuishia dukani akaingia chumbani Kwa mtumishi huyo na kuanza kukagua. Alikagua bila kufuata utaratibu unaotakiwa.Hakuwa na mwenyekiti wala mjumbe wa serikali ya mtaa!

Kule chumbani hakuambulia chochote.Wakati wanamtoa mtuhumiwa (mtumishi husika)askari husika pamoja na mgambo walianza kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili pasipo sababu za msingi.Kufika kituoni askari aliita mgambo na kumvulisha nguo na kubaki na nguo ya ndani.

Mgambo aliyefanya haya anaitwa John.Kitendo kile cha udhalilishaji kilimtoa machozi askari mmoja wa kike aliyekuwa ndani na hasa baada ya kujiridhisha hapa kuwa na kesi ya msingi isipokuwa kulikuwa na namna!

Suala lile lilifika ofisi ya dci ambaye alilisukukma kwa RPC wa mkoa ambaye alituma watu toka ofisi ya RCO mkoa ambapo walifika na kumhoji mtuhumiwa kuhusu sakata lake.Alihojiwa ana Kwa ana na wapelelezi zaidi ya watano kupitia simu na njia za ana kwa ana!

Mpaka Leo mtuhumiwa kadhulumiwa tv yake na kila anapofuatilia tv hiyo ya chogo isiyo na buttons amekuwa akizungushwa tu. File lipo Kwa askari mmoja aitwaye mbijima!Huyu kila anapogiwa simu na mtuhumiwa huwa ana respond negatively. Kwa kifupi hiki kituo kifumueni tu sababu kukaa kwao Kwa muda mrefu kumewafanya wafanye kazi Kwa mazoea na siyo kufuata taratibu!

Maelezo ya ziada
Kilichokuja kubainika hiyo kesi haikuwa na mlalamikaji. Lakini pia baada tu ya mtumishi huyo kufikishwa kituoni yule kichaa aliachiwa huru muda uleule.Huku mtumishi husika akibaki na kudhalilisha. Hivi inakuwaje aliyeuza tv atolewe wakati ni sehemu ya ushahidi?Ukweli polisi wananyanyasa sana raia wema na kuacha wahalifu wakidunda. Makamishna wa polisi makao makuu hebu fuatilieni hili tukio mtapata picha ya uonevu WA baadhi ya askari Kwa raia wema

Itaendelea......
 
Back
Top Bottom