Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,428
- 3,937
Miaka ya hivi karibuni kumetoka tabia ya viongozi wa serikali mara kwa mara kutoa kauli za ovyo zisizo na staha zinazoleta ukakasi katika jamii ila kwa sababu hatuna uwajibikaji, tatizo hilo tumeendelea kulilea.
Nilikuwa naangalia clip moja ya hivi karibuni ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akiongelea masuala ya ajira, akasema hivi "Hauwezi kujiajiri kwa jina la Roho Mtakatifu, you have to prepare".
Bwana Bashe ni mtu ambaye nimekuwa namuona anaongea kwa kufikiri na umakini tofauti na viongozi wengine kwa hiyo nilishtuka nilipoisikia hii kauli yake. Nilisita hata kuleta huu uzi ila nimeona niandike hivi kwa faida yake na viongozi wengine. Kwa mtazamo wangu akirekebisha kauli hii itakuwa mfano mzuri kwa viongozi wengine ambao huwa hata hawarudi kuomba radhi pale wanapotoa kauli za kuudhi.
Nimkumbushe Bwana Bashe kuwa ni muhimu sana akawa sensitive na imani za watu wengine. Katika Ukristo, dhambi ambayo HAISAMEHEKI ni kutoa maneno ya kejeli au kashfa dhidi ya Roho Mtakatifu (Mathayo 12:31-32).
Kipande cha video hiki hapa chini.