Mungu wenu wa kulialia na kuomba msaada.
Pale juu ya msalaba wahuni walipomtundika alikua analia kama mtoto alonyimwa peremende.
pale alikuwa amevaa mwili wa mwanadamu, na Roho ile ya kimungu ilikuwa imemwacha ili apate maumivu sawasawa na yale ambayo wanadamu huwa tunapata, aaibishwe sawaswa na sisi wanadamu tunavyoaibishwa, ili akipata maumivu sisi tusipate maumivu kama tukimwamini. ilikuwa lazima ayapate yale, na hata hayo uliyoyataja sio hayo tu aliyoyapata; angalia hapa chini;
1.
walipomkamata walimvuta ndevu hadi damu zikatoka usoni. ili wewe usifanyiwe hayo.
2.
walimtemea mate usoni kwa dharau. ili wewe na mimi tusiaibishwe through him.
3.
walimvua nguo na kuaibishwa. ili mimi na wewe tusiaibishwe. alibeba aibu yetu.
4.
walimpiga mijeledi yenye misumari, damu nyingi ikamtoka. kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
5.
walimdhihaki na kumwambia ajiokoe, sawasawa na vile wewe unamdhihaki leo. ili mimi na wewe tusidhihakiwe.
6.
walimpigilia misumari mikononi, damu nyingi ilimtoka. kwa mikono yetu hiihii, kama ukimwmaini Yesu, utaweka mikono juu ya wagonjwa, nao watapata afya. hakuna mtume mwengine au nabii au masihi ambaye anaweza kuponya hata uywele mmoja tu. wote longolongo tu, ila kwa Jina la Yesu, watu wanapona tukiwawekea mikono yao na majini yanawakimbia.
7.
walimpigilia misumari miguuni, damu nyingi ilimtoka.popote tunapokanyaga Mungu yupo nasi na tunao uwezo kumkanyaga nyoka nge na nguvu zote za shetani wala hakuna kitakachotudhuru tukiwa ndani yake.
8.
walimvika taji ya miiba kichwani, damu nyingi ikamtoka. Miiba ni ishara ya laana, yeye alilaaniwa badala yetu, alibeba laana ili kuondoa laana kwa wote watakaomwamini. kuishi na laana sasaivi ni uamuzi wako tu ila yupo aliyelipa garama ya laana zako, Yesu Kristo pekee.
9.
alikufa, na wakamchoma mkuki ubavuni, damu na maji vikatoka. damu na maji ni udhihirisho wa mtu aliyekufa, hivyo alikufa kweli. Mauti na kuzimu hazina nguvu kwa walio katika Kristo Yesu. ukifa umekufa kwasababu Mungu ametaka, ila mashetani, majini wachawi n.k hawana uwezo kukuua kama upo ndani yake, kwasababu Yesu Kristo alishinda mauti na kuzimu kwa kufufuka kwake.
10. siku ya tatu alifufuka na alipaa mbinguni, yu hai hata leo na ni mwokozi wa ulimwengu.
bahati mbaya, mitume wengine wote na manabii au wale mnaowaamini, hawakufa kwa ajili yenu.
zamani zile, au niseme asili ya Mungu ilivyo, ni kwamba hakuna ondoleo la dhambi/hakuna kusamehewa hadi damu imwagike. zamani ili kusamehewa dhambi ilikuwa lazima utoe kafara la wanyama, uwachinje uwachome ndio wawe wamekufa kwa ajili yako. lakini ikawa watu wasio na wanyama au wale masikini kama wewe wasingeweza kuwa na wanyama kila wakati kuchinja kwa ajili ya dhambi zao, kwasababu ziko nyingi. pia, kafara la wanyama lilikuwa kwa ajili ya kufunika tu dhambi ila sio kuondoa.
Mungu tangu awali akawa amefanya mpango kwamba, iwepo kafara moja tu once and for all, itakayotumiwa na wanadamu sio mmoja au wawili, bali wote dunia nzima, wale watakaoliendea hilo kafara dhambi zao zisamehewe kwasababu kafara hilo lilibeba dhambi zote. garama yake ilikuwa kubwa kulipa madeni yote ya dhambi. ndio akawa reincanated (roho kufanyika mwili), akaingia kwa njia ya Roho Mtakatifu ndani ya tumbo la maria ili azaliwe kama mwanadamu, aishi kama mwanadamu, ayashinde yote ya maisha ya mwanadamu na kuyashinda, na alipofikia miaka 33 pasipo kufanya dhambi yeyote, akiwa mtakatifu, damu yake ikamwagika badala ya dhambi za ulimwengu wote ili yeyote atakayemwendea apate ticket ya kusamehewa dhambi bila kulipa garama nyingine. ndio akateswa na kuumizwa kama hapo juu nilivyokuelezea.
hapana jina lingine liwalo lote lile tulilopewa sisi wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo, ila Jina la Yesu Kristo. hilo ndilo jiwe lililokataliwa na ninyi waashi, lakini ndio jiwe kuu la pembeni/jiwe la msingi. bila msingi huo humwoni Mungu. Kwa Jina la Yesu kila goti litapigwa la vitu vilivyoko mbinguni, duniani na chini ya nchi, na kila ulimi utakiri ya kwamba Yesu Kristo ni Bwana.
Yesu Kristo ndiye njia kweli na uzima, mtu haji kwa Baba ila kwa njia yake tu. hakuna mtume wala nabii mwingine aliteswa na kuuawa kwa ajili yako, na hakuna mwingine aokoaye ila yeye tu.
Yesu Kristo anakupenda sana. soma Isaya 53, alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu, adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisit umepona. Isaya 52 mwishoni utaona jinsi ilivyowashangaza wengi, wafalme na wakuu na watu wa dunia namna alivyokuwa, kwasababu alizaliwa na kuishi kama mtu mwororo/dhaifu, hakuna mtu ambaye unaweza kumdhania kuwa ndiye mwokozi wa ulimwengu. Biblia inasema hata ukimtazama hakuwa mtu anayetamanisha kumtazama kwasababu alikataliwa na watu. alikuwa mtu wa huzuni nyingi ajuaye sikitiko. uzuri ni kwamba, alihuzunika hadi hatua ya mwisho kabisa akawa amebeba huzuni zetu zote ili mimi na wewe tukimwamini tusibebe mzigo wa huzuni, alidharauliwa hadi na kila mtu ili mimi na wewe tusidharaulike, uliuchukua udhaifu wetu wote, na kwakupigwa kwake sisi tumepona.
maneno haya unayoyasoma, kama hautamwamini Yesu Kristo na kuyaponya maisha yako, kuna siku utayakumbuka na itakuwa too late for you. namwomba Mungu akusaidie umrudie yeye na uache njia mbaya, uache kufuata mitume na manabii waongo ambao hawakufa kwa ajili yako.