elivina shambuni
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 461
- 295
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo amekerwa na utendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mbinga vijiji kwa kuchelewa kukamilisha ujenzi wa kituo cha Afya Mapera.
Jafo ametoa siku 17 majengo yote ya kituo hicho yawe yamekamilika.
Kituo hicho kilipokea fedha mwezi Mei 2019 na kutakiwa kukamilika mwezi Novemba 2019 lakini ujenzi wake bado haujakamilika.
Kitendo hicho kilisababisha waziri huyo kuwa mbogo na kuwataka wasimamizi wa halmashauri hiyo kukamilisha kituo hicho kabla tarehe 15/01/2020 yaani siku 18 kutoka sasa.
Kilichomkera zaidi ni pale alipokuwa baadhi ya mafundi aaliopewa kazi hiyo kutokuwepo site yaani kazi zao zimesimama wakati majengo bado hayaja kamilika.
Wakati huo huo Waziri Jafo amewapongeza sana halmashauri ya Mji wa Mbinga kwa kujenga jengo zuri la halmashauri hiyo ndani lililojengwa ndani ya muda.
Jengo hilo lililojengwa na SUMAJKT limemerahisha utendaji wa kazi na Waziri Jafo ameelekeza watumishi wa halmashauri hiyo kuingia katika Ofisi zao za Kisasa mwanzoni mwa mwaka mpya yaani Januari 2020.
Jafo amesisitiza kwamba anataka watumishi wajitume kwa maslahi mapana na Nchi na wananchi wake.