Waziri Jafo: Kila manispaa mkoani DSM itarithi mali za Jiji la Dar es Salaam lililovunjwa zilizo katika maeneo yao

Waziri Jafo: Kila manispaa mkoani DSM itarithi mali za Jiji la Dar es Salaam lililovunjwa zilizo katika maeneo yao

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa Tamisemi Mh. Jaffo amesema mgawanyo wa mali za lililokuwa jiji la Dar es salaam ambalo limevunjwa utakuwa kwamba kila manispaa itarithi mali zilizo katika maeneo yao ya kiutawala.

Kwa mfano stendi ya mabasi ya mkoani yaani Stendi ya Magufuli itarithiwa na manispaa ya Ubungo nk nk!

Maendeleo hayana vyama!
 
Mnyika alifubaza sana maendeleo ya Ubungo tungekuwa mbali.
 
Ingependeza kila halmashauri ingerithi viwanja eneo husika walau vya michezo baada ya taifa kuingia mfuko wa vyama vingi.
 
Waziri wa Tamisemi mh Jaffo amesema mgawanyo wa mali za lililokuwa jiji la Dar es salaam ambalo limevunjwa utakuwa kwamba kila manispaa itarithi mali zilizo katika maeneo yao ya kiutawala.

Kwa mfano stendi ya mabasi ya mkoani yaani Stendi ya Magufuli itarithiwa na manispaa ya Ubungo nk nk!

Maendeleo hayana vyama!
Halafu Bwashee mwambie Mzee wako atatuharibia Nchi sasa kwa majina ya watu! Yaani kila kitu kinaitwa jina la mtu! Nongwa tu awe ni rafiki au mentor wake! Flyovers zinaitwa majina ya watu! Barabara majina ya watu!

Utashangaa hadi treni ya mwendokasi nazo ataziita majina ya watu! Mwisho wa siku mpaka majina ya Mikoa, Wilaya, Tarafa, Kata hadi Kijiji! Yataitwa majina ya watu!

Hivi kuna ulazima kiasi hicho! Mfano mdogo tu hapajuzi kati tuliambiwa Stendi yaMabasi ya Korogwe itaitwa jina la Katibu Mkuu Kiongozi aliyefariki John Kijazi! Hatujakaa sawa, mmempa na hiyo Ubungo Interchange!! Kulikoni nyinyi watu!
 
Waziri wa Tamisemi mh Jaffo amesema mgawanyo wa mali za lililokuwa jiji la Dar es salaam ambalo limevunjwa utakuwa kwamba kila manispaa itarithi mali zilizo katika maeneo yao ya kiutawala.

Kwa mfano stendi ya mabasi ya mkoani yaani Stendi ya Magufuli itarithiwa na manispaa ya Ubungo nk nk!

Maendeleo hayana vyama!
Nani atarithi DAWASA?

Amandla...
 
Hivi kila kitu wanaita mMagufuli, jina baya hivi kweli
 
Back
Top Bottom