Kwanza nitoe pongezi zangu za dhati kwako kwa ufanyaji kazi wako uliotukuka.
Jafo naomba upatapo ujumbe huu ufanyie kazi; sio nakulazimisha mzee wangu hapana ni sehemu ya uzalendo wa vijana wako waliokuwa chini ya Halmashauri mbali mbali.
Waziri, vijana wengi wameajiriwa ndani ya Halmashauri nyingi kwa mkataba yaani temporary kwa ajili ya kukusanya mapato au ushuru ndani ya vyanzo vya mapato vya halmashauri. Ni ukweli usiopingika vijana wengi waliokuwa huko sio kwamba hawana Elimu, wengi ni Degree holders na Diploma holders.
Waziri tatizo ni mishahara au posho wanazolipwa lakini ukiangalia kwa undani hawa ni WAZALENDO Kama walivyokuwa vijana wa JKT. Waziri naamini kabisa una ushawishi mkubwa sana kwa Rais wa JMT ili vijana hawa wapate ajira za kudumu au waongezewe posho na kuwekewa misingi ambayo wanaweza kupata mikopo kwenye mabenki kama wafanyakazi wengine wa Halmashauri zetu kwani wanakusanya mapato mengi ambayo yanatusaidia kujenga Taifa letu.
Waziri Jafo na viongozi wengine tunawaomba mumshauri Raisi wetu wa JMT Dkt. John Magufuli au mumpe taarifa ili aweze kutufikiria sisi vijana wake.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika na Viongozi wote. Amina