Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
January Makamba akijibu hoja za wabunge kuhusu kukatika kwa umeme, kwanza alimlaumu mbunge Musukuma kwa kumshambulia yeye binafsi na kueleza kazi ya ubunge sio kushambuliana na kama ana matatizo na yeye kuwa waziri au samia kuwa rais apeleke kwingine lakini sio kwenye masuala ya nchi.
Pamoja na maelezo mengine, Makamba alitoa takwimu za TRA zinazoonyesha kipindi cha urais wa Samia suluhu na yeye akiwa waziri, makusanyo yamepanda, na kueleza hii inatokana na kuwa wao hawawakatii wenye viwanda umeme na kuwaambia wanyamaze ndio maana uzalishaji umepanda.
Makamba aliongeza pia matatizo ya kukatika kwa umeme yametokana na legacy, ambapo kipindi kilichopita repair and maintainance ilikuwa haifanywi ipasavyo, na akamaliza kwa kusema kama waziri aliyepita alipewa miaka 4, basi na yeye apewe miaka 4 waone kama hali ya kukatika itakuwepo na kama Magufuli walimpa miaka 6 basi na Samia wampe miaka 6 waone kama haya matatizo yatakuwepo