Waziri January Makamba anamaanisha Magufuli alikuwa akiwakatia umeme watumiaji wakubwa na kuwatisha wakae kimya?

Waziri January Makamba anamaanisha Magufuli alikuwa akiwakatia umeme watumiaji wakubwa na kuwatisha wakae kimya?

Aise jamaa ni mpumbavu huyu, yaani imetoka tu awamu ya 5 ghafla umeme unaanza kukatika, halafu anatoa visingizio eti hapakuwa na maintance, hivi mitambo mikubwa namna ile uendeshe miaka 6 bila maintanance na isife??!!!, hivi anatuonaje huyu jamaa..?!
 
Baada ya mitambo haikufanyiwa service miaka mitano,leo wanasema hichi tena
 
Sauti ya makamba inatosha kbsa haina haya ya kuongeza
Waziri kashasema na uwo ndo msimamo wa wizara na ukwel ndo huwo kausema sasa Sukuma gang na msukule wenu pambanen
Tulia ww Id ya mkakati,usitufatie ban
 
January Makamba akijibu hoja za wabunge kuhusu kukatika kwa umeme, kwanza alimlaumu mbunge Musukuma kwa kumshambulia yeye binafsi na kueleza kazi ya ubunge sio kushambuliana na kama ana matatizo na yeye kuwa waziri au samia kuwa rais apeleke kwingine lakini sio kwenye masuala ya nchi.

Pamoja na maelezo mengine, Makamba alitoa takwimu za TRA zinazoonyesha kipindi cha urais wa Samia suluhu na yeye akiwa waziri, makusanyo yamepanda, na kueleza hii inatokana na kuwa wao hawawakatii wenye viwanda umeme na kuwaambia wanyamaze ndio maana uzalishaji umepanda.

Makamba aliongeza pia matatizo ya kukatika kwa umeme yametokana na legacy, ambapo kipindi kilichopita repair and maintainance ilikuwa haifanywi ipasavyo, na akamaliza kwa kusema kama waziri aliyepita alipewa miaka 4, basi na yeye apewe miaka 4 waone kama hali ya kukatika itakuwepo na kama Magufuli walimpa miaka 6 basi na Samia wampe miaka 6 waone kama haya matatizo yatakuwepo

Yaani kwa kauli hii huyu jamaa nimemtoa maana mazima. Hajui uonvozi bali anabebwa na jina la baba yake. Hawa watu kula kulala kwa baba wakipata madaraka ni shida mnoo. Halacu anainviza jina la Samia hapo ili iweje? Au anatembelea nyota yake? Jamaa kaprove failure kwa kweli.
 
Acheni kelele.. Hii wizara ina changamoto nyingi na hazijaanza leo wala jana.

Too early kumjudge vibaya Makamba aliyepewa wizara muda mfupi uliopita.

Nasisitiza ni mapema mno apewe muda zaidi..
Kama wizara ina changamoto nyingi basi ni vema huyo makamba akajikita kutatua changamoto hizo na kujibu maswali ya watu, maana yeye ndie aliepewa wizara. Masuala ya kukatika viuno na kuimba ngonjera bungeni, hilo ni big no. Kaprove failure huyo jamaa yenu.
 
Watanzania wengi hawujui chochote kuhusu umeme na mikataba zaidi ya kwamba ni wahanga wa uwongo wa Magufuli. Na kwa ujinga wao ndiyo walikuwa mtaji wa Magufuli kwa miaka 5.

JNHPP was wastage of money. Hilo dude litabakia white elephant. Litajengwa ila halitakuja kuzalisha hizo megawati 2,100 za umeme.

Kwa maamuzi ya Dikteta mmoja mkemia asiyeamini sayansi, tumeharibu baioanuai ya selous na kukata miti yenye saizi ya ukubwa wa Mkoa wa Dar es Salaam. Hili litatugharimu milele.

Ni wakati wa kufanya maamuzi magumu kwa kusitisha kuendelea kujenga na kuendelea na umeme wa gesi. Kwa sasa Kinyerezi 1 & 2 zinachangia 60% ya umeme tunaotumia Tanzania. Na zinatumia hardly 10% ya gesi ya Mtwara

Miradi yote ya maji yaani Kidatu, Mtera, Kihansi, Nyumba ya Mungu, Hale, Pangani nk inachangia 40%. Numbers don't lie. Umeme wa kutegemea mvua siyo reliable na vile vile una athari kwa mazingira.

Kama Magufuli asingetokea mwaka 2015 tungepiga hatua kubwa sana kiuchumi kwa kuwa;
1. Kinyerezi 3 & 4 zingekamilika na kuwa chanzo kikuu cha nishati.

2. Tusingevuruga baioanuai ya Selous kwa kukata miti ili tujenge bwawa la umeme kwa ajili ya kupata Megawati 2,100 tu ambazo zinapatikana kwa kutumia 25% tu ya gesi ya Mtwara.
Inaonekana wewe ndio hujui lolote kuhusu umeme.
 
Nyield bhana na genge lenu mna mambo sana

Anyway,lakini kama JIWE aliweza kumtoa hadharani aliekua waziri wake wa mipango akiwa mgonjwa hoi aje awathibitishie watu mbele za camera kua haugui covid-19 sasa atashindwaje hilo unalolisema???

Busara kwenu kwa moment hii ni nyie kukaa kimya tu na wapeni air time wenye moment yao
 
January Makamba akijibu hoja za wabunge kuhusu kukatika kwa umeme, kwanza alimlaumu mbunge Musukuma kwa kumshambulia yeye binafsi na kueleza kazi ya ubunge sio kushambuliana na kama ana matatizo na yeye kuwa waziri au samia kuwa rais apeleke kwingine lakini sio kwenye masuala ya nchi.

Pamoja na maelezo mengine, Makamba alitoa takwimu za TRA zinazoonyesha kipindi cha urais wa Samia suluhu na yeye akiwa waziri, makusanyo yamepanda, na kueleza hii inatokana na kuwa wao hawawakatii wenye viwanda umeme na kuwaambia wanyamaze ndio maana uzalishaji umepanda.

Makamba aliongeza pia matatizo ya kukatika kwa umeme yametokana na legacy, ambapo kipindi kilichopita repair and maintainance ilikuwa haifanywi ipasavyo, na akamaliza kwa kusema kama waziri aliyepita alipewa miaka 4, basi na yeye apewe miaka 4 waone kama hali ya kukatika itakuwepo na kama Magufuli walimpa miaka 6 basi na Samia wampe miaka 6 waone kama haya matatizo yatakuwepo

Sijawahi elewa kwa nini watu Wana chuki binafsi na Makamba JR.

Jambo la pili,akina Msukuma kwa nini wasiende Tanesco wapate maelezo ya kwa nini umeme unakatika?
 
Makamba mpuuzi kweli, anamuingiza Rais kwenye masuala ya wizara yake kama kichaka cha kuficha udhaifu wake, lazima awe accountable kama kazi imemshinda apishe wengine.

Urais wa Samia unahusika nini na kukatika umeme?

Divide and conquer

Hapo anataka kuonyesha ni vita kati ya sukuma vs msoga
 
Hii nchi ni ngumu kusonga, uzuri nje ya haya malalamiko tutamkumbuka Mzee Warioba na timu yake kama watu waliona ubovu wa katiba iliyopo na umuhimu wa katiba mpya.

Naamini uchaguzi wa 2019 na wa 2020 ungelikuwa huru na haki upuuzi mwingi usingelikuwepo sasa ila cha kuchekesha wanaolalamika sasa ni waliochekea wizi wa uchaguzi, na hilo liwe funzo kuanzia sasa. Waacheni wale urefu wa kamba zao, misita tena
Tunasingizia Katiba kana kwamba ndio inayotenda. Ni sawa na mwanadamu anayemsingizia Mungu kwa matendo yake
 
January Makamba akijibu hoja za wabunge kuhusu kukatika kwa umeme, kwanza alimlaumu mbunge Musukuma kwa kumshambulia yeye binafsi na kueleza kazi ya ubunge sio kushambuliana na kama ana matatizo na yeye kuwa waziri au samia kuwa rais apeleke kwingine lakini sio kwenye masuala ya nchi.

Pamoja na maelezo mengine, Makamba alitoa takwimu za TRA zinazoonyesha kipindi cha urais wa Samia suluhu na yeye akiwa waziri, makusanyo yamepanda, na kueleza hii inatokana na kuwa wao hawawakatii wenye viwanda umeme na kuwaambia wanyamaze ndio maana uzalishaji umepanda.

Makamba aliongeza pia matatizo ya kukatika kwa umeme yametokana na legacy, ambapo kipindi kilichopita repair and maintainance ilikuwa haifanywi ipasavyo, na akamaliza kwa kusema kama waziri aliyepita alipewa miaka 4, basi na yeye apewe miaka 4 waone kama hali ya kukatika itakuwepo na kama Magufuli walimpa miaka 6 basi na Samia wampe miaka 6 waone kama haya matatizo yatakuwepo

Makamba tunamjua ni mpigaji yeye anachotaka zile mashine za kutumia mafuta zifanye kazi watu wale maisha.
 
Ungese mtupu umeandika, unajua cost za umeme wa gas? Na gas yenyewe tunanunua sio yetu. JNHPP ndo suluhisho pekee shida ya wabongo tunadandia tu,

Kwani kitu kikiwa chetu ndio kinakuwa bei rahisi? Ndege za ATCL ni zetu, mbona sio nafuu kama ilivyokuwa fastjet? Mbona cement na sukari zinazozalilishwa hapa hapa kwetu sio bei rahisi kama za nje?
 
Ns swali kaulizwa yeye km waziri anamchomekea Samia wa nini.
Eti km una chuki na mimi au mama Samia.
Jibu swali kuhusu kukatika kwa umeme kiholela full stop.

Sasa hivi ni fashion kila mwanaccm akiongea anamtaja rais, siasa hizi za kipuuzi zilipandikizwa kipindi cha utawala wa kidhalimu wa Magu.
 
Mbunge musukuma hajaanza leo kuwabwatukia mawaziri.aliwahi pia kumbwatukia waziri mpina wa mifugo na uvuvi kpnd cha awamu ya jana..lakn reaction ya makamba imekuwa tofauti..ukimgusa, eti unamwonea wivu!
 
Hizi ndio akili za waziri, anaongea utafikiri yupo kwenye kampeni za uchaguzi, hakuna fact yoyote kwa majibu anayotoa.
makamba yuko sahihi kumbe mwendazake aliwakatia wenye umeme viwanda ili mgao usionekana,jamaa alikuwa mjanja sana,jamaa kiboko
 
Musukuma yeye ni La Saba oyee. Kwa mujibu wake yeye mwenyewe. Hii PhD anayotamba nayo ni swagger Tu. Tusiyumbe tukamuita msomi. Tutafeli
ameshawaambia wenyewe hawatawakatia wenye viwanda umeme ili kuficha mgao wa umeme ,nini ambacho hamuelewi enyi uzao wa nyoka
 
Sasa hivi ni fashion kila mwanaccm akiongea anamtaja rais, siasa hizi za kipuuzi zilipandikizwa kipindi cha utawala wa kidhalimu wa Magu.
Bado anakuchapa hata baada ya kufa?
 
Back
Top Bottom