Waziri Japhet Hasunga: Serikali kuanzisha Mamlaka rasmi itakayosimamia mazao ya mboga na matunda nchini (Horticulture)

Waziri Japhet Hasunga: Serikali kuanzisha Mamlaka rasmi itakayosimamia mazao ya mboga na matunda nchini (Horticulture)

Lakini Pascal kuna ujinga flan kwenye hii nchi. Kila zao lililoanzishiwa board au mamlaka basi zao hilo limeishia pabaya sana. Mfano:
1. Board ya Korosho hamna inachofanya kwenye korosho zaidi ya wizi, ufisadi na kulipana posho.

2. Bodi ya kahawa ni hivyo hivyo
3. Boadi ya pamba ni hivyo hivyo
4. Bodi ya katani ni hivyo hivyo
5. Bodi ya tumbaku ni hivyo hivyo
6. Bodi ya chai

Kimsingi bodi zote za mazao zimekuwa sehemu ya kuhalalisha dhuluma dhidi ya wakulima masikini ambao hata kwenye hizo bodi huwa hawana nafasi ya kuwakilishwa na kusikilizwa kero zao.

Sijui hii ya "hortculture" sababu ina wadau wengi ngozi nyeupe hawatakubali ujinga.

Mi nataka kusema zao lolote likianzishiwa bodi nchini ndiyo linakuwa limeanza safari yake ya kuzimu.

Bora mazao yawe huru bila bodi. Mbona hawanzishi bodi ya mahindi, au ulezi au ndizi au mchele? Hayo yote tunaexport.

Nasubiri wakiona wakulima wa maparachichi tunamake sana hela watatuanzishia bodi ya maparachichi
Binafsi siyo shabiki mzuri wa hizi bodi/agency. Inatosha sana kuwa na idara/kitengo tu wizarani kinachosimamia tasnia/subsector husika.

Kuanzisha hizo bodi huambatana na "upuuzi" ufuatao.

1. Kuongeza urasimu kwa wadau (wakulima, wafanyabiashara,nk) pale wanapotaka kusajili au kufanya shughuli zao; it's all about vibali!

2. Kuongeza idadi ya tozo/kodi kwa mazao husika. Hizo agency mara nyingi haziendeshwi na serikali kuu hivyo hutegemea tozo mbalimbali na "faini" kutoka kwa wadau zinaowasimamia kama chanzo kikuu cha mapato.

3. Kupunguza tija (productivity) ya serikali as a whole kwa kuweka msururu wa watu au vitengo au idara zinazosimamia au kuratibu kitu kile kile kimoja!

That way utaona kuwa badala ya kuwa na positive effect, kuzaliwa kwa taasisi kama hizi huwa na negative effect kwa "zao" husika.

Hao TAHA wamedai agency "yao" kwa kuwa kuna vitu wanakosa. Waziri wetu wa kilimo angekuwa "waziri wa kilimo" angepambana ahakikishe wanapata wanavyotaka na si kuongeza utitiri wa taasisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom