Waziri Japhet Hasunga: Serikali kuanzisha Mamlaka rasmi itakayosimamia mazao ya mboga na matunda nchini (Horticulture)

Binafsi siyo shabiki mzuri wa hizi bodi/agency. Inatosha sana kuwa na idara/kitengo tu wizarani kinachosimamia tasnia/subsector husika.

Kuanzisha hizo bodi huambatana na "upuuzi" ufuatao.

1. Kuongeza urasimu kwa wadau (wakulima, wafanyabiashara,nk) pale wanapotaka kusajili au kufanya shughuli zao; it's all about vibali!

2. Kuongeza idadi ya tozo/kodi kwa mazao husika. Hizo agency mara nyingi haziendeshwi na serikali kuu hivyo hutegemea tozo mbalimbali na "faini" kutoka kwa wadau zinaowasimamia kama chanzo kikuu cha mapato.

3. Kupunguza tija (productivity) ya serikali as a whole kwa kuweka msururu wa watu au vitengo au idara zinazosimamia au kuratibu kitu kile kile kimoja!

That way utaona kuwa badala ya kuwa na positive effect, kuzaliwa kwa taasisi kama hizi huwa na negative effect kwa "zao" husika.

Hao TAHA wamedai agency "yao" kwa kuwa kuna vitu wanakosa. Waziri wetu wa kilimo angekuwa "waziri wa kilimo" angepambana ahakikishe wanapata wanavyotaka na si kuongeza utitiri wa taasisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…