Waziri Kabudi: Viongozi wa dini ambao hawajasajiliwa na RITA hawataruhusiwa kufungisha ndoa ya aina yoyote

Waziri Kabudi: Viongozi wa dini ambao hawajasajiliwa na RITA hawataruhusiwa kufungisha ndoa ya aina yoyote

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amesema viongozi wa dini ambao hawajasajiliwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) hawataruhusiwa kufungisha ndoa ya aina yoyote na endapo watafungisha ndoa bila ruhusa, ndoa hiyo itakuwa batili.

Kabudi.jpg
 
Hao wafungishwa ndoa watawajuaje sasa, anyway hilo linaeleweka kuwa ndoa ya ikfungishwa na mtu asiye na mamlaka manake ni batili from the way go
 
SHERIA ILIKUWA HIVYO MIAKA YOTE.
WACHUNGAJI NA MAASKOFU LAZIMA WAWE NA LESENI YA:

1. KUFUNGISHA NDOA
2. KUONGOZA MAZISHI.

SASA HUYU KABUDI NADHANI ANATUKUMBUSHA TU.
 
Kabudi tangu aingie kwenye siasa alisahau na taaluma yake
Sharti la kupewa uongozi na CCM ni lazima ukabidhi ubongo wako kwa mwenyekiti na bichwa lako libaki tupu halafu watakuwekea makororo mengine.
 
Hivi misukule inayofufuliwa pale Kawe, RITA wanaizingumziaje ? Wanawatambua kama waliofariki au wanawahesabia wamezaliwa upya ?
Hili ini swali zuri sana kuwauliza wenye mamlaka ya kulinda sheria zetu na kutuepusha na matapeli.

Siyo hivi wanaongelea mambo ambayo hata walio chekechea wanajua. Au waliachia tu wamekuja kushtuka sasa?
 
Hivi misukule inayofufuliwa pale Kawe, RITA wanaizingumziaje ? Wanawatambua kama waliofariki au wanawahesabia wamezaliwa upya ?
haaha inabidi RITA ihakikishe vyeti vyao vya kifo vya hao misukule vinafutwa na kuwasajili kama raiya wa kigeni kutoka mashamba ya giningi.
 
Kibudu ameenda kwenye eneo lake. Huyu ni prof. wa Family Law (Ndoa na mirathi), ni branch ambayo inasomwa na wenye uwezo mdogo wa kimasomo.
 
Ndoa itakuwa batili mwenye kufungiwa ndoa atajuaje kuwa anayefungisha ndoa hajasajiliwa na RITA?
Kwanza vyeti vyote huwa vinatolewa na serikali so hataweza kuwa na cheti halali, labda ubuni chako as wale jamaa zetu.
 
Back
Top Bottom