Waziri Kairuki: Usajili wa Intaneti Tanzania Wafikia Milioni 62, ongezeko la 6%

Waziri Kairuki: Usajili wa Intaneti Tanzania Wafikia Milioni 62, ongezeko la 6%

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Idadi ya usajili wa intaneti nchini Tanzania imepata ukuaji mkubwa na kufikia 62,793,986 kufikia mwezi Juni 2026. Ukuaji huo unadhihirisha kasi ya mabadiliko ya kidijitali na kuongezeka kwa matumizi ya huduma za mawasiliano nchini.

Akiwasilisha Ripoti ya Hali ya Sekta ya Mawasiliano ya mwezi Juni 2026 jijini Dar es Salaam, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, ameeleza kuwa sekta hiyo imeendelea kuonyesha mwelekeo chanya wa ukuaji kwa kipindi cha kuanzia Machi 2025 hadi Juni 2026.

Mwenendo wa Ukuaji wa Usajili wa Intaneti (2025 – 2026)​

Katika taarifa yake, Waziri Kairuki alichanganua takwimu za ukuaji wa usajili wa intaneti kama ifuatavyo:

  • Machi 2025: Usajili wa intaneti ulikuwa na watumiaji 49,333,839.
  • Juni 2025: Baada ya miezi mitatu, idadi hiyo iliongezeka kwa 10% na kufikia watumiaji 54,078,000.
  • Septemba 2025: Usajili ulifikia watu 56,322,287, ikiwa ni ongezeko la 4% ikilinganishwa na mwezi Juni 2025.
  • Disemba 2025: Kasi ya ukuaji iliendekea kwa 3%, ambapo usajili ulifikia watumiaji 58,106,264.
  • Machi 2026: Usajili uliongezeka kwa 1% na kufikia watu 58,974,820.
  • Juni 2026: Katika ripoti ya hivi karibuni, usajili umekua kwa 6% na kufikia jumla ya watumiaji 62,793,986.
Soma Pia: Angellah Kairuki: Matumizi ya Internet yameongezeka kwa asilimia 19.5, watumiaji wafikia Milioni 58.9

 
Back
Top Bottom