johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Waziri wa nishati Dr Kalemani ameitaka Ewura kuhakikisha bei ya gesi ya majumbani inashuka ndani ya siku 14 kuanzia leo.
---
CHATO. Waziri wa Nishati nchini Tanzania Dkt. Medard Kalemani amemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) nchini kuhakikisha anashughulikia suala la kupandishwa kiholela kwa bei ya mitungi ya gesi ya majumbani nchini ndani ya kipindi cha siku 14 kuanzia hii leo Agosti 9, 2021.
Dkt.Kalemani ametoa agizo hilo hii leo Agosti 9, 2021 Wilayani Chato Mkoani Geita wakati wa uzinduzi wa kongamano la uzinduzi wa bomba la mafuta ghafi litakalojengwa kutoka Uganda mpaka Tanzania litakalogharimu kiasi cha USD 3.2.
Dkt. Kalemani amewataka Wakurugenzi wa EWURA pamoja TPDC kuweka matangazo yao ya kazi kwa lugha ya kiswahili ili kuepukana na changamoto ya wasiojua lugha ya Kiingereza.
Hivi juzi mitungi ya Gesi zote za majumbani iilipanda bei kwa wastani wa zaidi ya asilimia 12.3 kuanzia mitungi midogo ya kati hadi Mikubwa kabisa, kiasi ambacho kilizua taharuki kwa jamii ambayo inatumia gesi hasa mijini.