Waziri Kalemani: Umeme ukikatika eneo lako toa taarifa, mameneja wa wilaya wakizembea siku 15 nawashusha vyeo

Waziri Kalemani: Umeme ukikatika eneo lako toa taarifa, mameneja wa wilaya wakizembea siku 15 nawashusha vyeo

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akikagua Miundombinu ya Umeme eneo la Ntyuka Jijini Dodoma 1 Aprili 2021, amewataka Wananchi kutoa taarifa sahihi na mapema pale Umeme unapokatika katika maeneo yao ili TANESCO iweze kuwafikia haraka na kurejesha Umeme mapema.

unnamed.jpeg

Waziri Kalemani ameeleza kuwa, hali ya upatikanaji wa Umeme nchini kwa sasa ni shwari na Umeme upo wa kutosheleza mahitaji baada ya kukamilika kwa matengenezo na ukarabati mkubwa wa mitambo mikubwa ya kuzalisha Umeme Nchini.

===
UMEME UKIKATIKA KWENYE ENEO LAKO TOA TAARIFA, MAMENEJA WA WILAYA NTAWASHUSHA WASIPOTIMIZA WAJIBU KWA SIKU 15.

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akikagua Miundombinu ya Umeme eneo la Ntyuka Jijini Dodoma 1 Aprili 2021, amewataka Wananchi kutoa taarifa sahihi na mapema pale Umeme unapokatika katika maeneo yao ili TANESCO iweze kuwafikia haraka na kurejesha Umeme mapema.

Waziri Kalemani ameeleza kuwa, hali ya upatikanaji wa Umeme nchini kwa sasa ni shwari na Umeme upo wa kutosheleza mahitaji baada ya kukamilika kwa matengenezo na ukarabati mkubwa wa mitambo mikubwa ya kuzalisha Umeme Nchini.
 
Ahsante sana,

Kwanza napenda sana kumpongeza Mhe. Waziri Dr. Kalemani. hongera sana.
Hakika ktk mawaziri wachapa kazi na wafuatiliaji Dr. Kalemani ni mmoja wao, hakika nimekubali kweli ni Mkufunzi wa Hayati JPM.

Mameneja wa wilaya na Mikoa na watendaji wao wa chini ndio tatizo kubwa, yaaani hawana muda wa kutembelea na kukagua miundo mbinu ya umeme, haitoshi tu kuagiza, kiongozi unatakiwa uwe mtu wa field kama alivyo waziri. unakuta umeme hauna nguvu, transfoma imeunganishwa kuzidi uwezo wa transfoma lenyewe!! hawana habari wao ni kutuma tu.

Nchi yetu ili isonge kwenda ktk uchumi wa daraja la juu lazima nishati iwe ya uhakika na ya kutosha kinyume chake tutakuwa tuna danganyana.
 
Isee nashangaa sana hawa matanesco hawaogopi kabisa, fikiria huku kwa makamu wa rais umeme unakata kata kila siku hata bila ya taarifa au sbabu ya kueleweka.

Mr kaleman Huku Buhigwe kuna shida pia, umeme unakata kata hovyoo, sasa sijui mantiki ya kutoa huduma hii kwa mwananchi.# Tanesco buhigwe mna shida
 
kalogwa huyu siku 15 hajui ni nusu mwezi huu afanye siku 5 kama kweli ana lengo la maana
 
Ati ?! Watoe taarifa wapi wahusika watashushwa vyeo? Ni mimi sijaelewa ama !! Hii nchi haishi mazingaombwe
hana akili huyu bwana, iyo taarifa anapewa nani na izo siku anahesabu nani? alafu katoa siku 15 si nusu mwezi kabisa huyu kadata
 
Sasa inakuwaje wananchi tutoe taarifa TANESCO wakati waliokata umeme ni hao hao TANESCO na taarifa wanayo tayari!
Mkuu sio kila Outage ni Planned, Kuna Unplanned outage ambazo mostly ni emergency kama nguzo kudondoka au Mti kudondokea laini
 
Mkuu sio kila Outage ni Planned, Kuna Unplanned outage ambazo mostly ni emergency kama nguzo kudondoka au Mti kudondokea laini
Hizo tunazijua na zipo kila siku, wala haikuhitaji kauli ya waziri. Lakini angalia vizuri alichosema, amesema 'umeme ukikatika', labda kama amenukuliwa vibaya
 
Siku 15 yaani kabisa anaona ni sawa muda wote huo?
 
Huyu Mchato imekuaje mpaka leo bado yupo katika hiyo wizara? Alipaswa abaki kuwa mbunge tu
 
Heri yao wenye umeme ambao wanatakiwa watoe taarifa!!! Sie wengine tuko manispaa kabisaa na HAKUNA hata nguzo ya umeme [emoji134][emoji134][emoji134][emoji134]
 
Kalemani tushamzoea too much maneno.
Mara Kama hujavuta umeme nakupeleka lock up.
Mara mameneja wafanyiwe uchunguzi ukikamilika nawapeleka mahakamani
Leo hii eti tuwapigie Tanesco. Muulizeni huyu msomi Ni lini Tanesco walipokea simu?
Kama haamini apige simu Tanesco Kibaha siku yoyote ikipokelewa namuwekea bando la wiki huyo atakae pokea.
Tanesco Kibaha. Pwani
 
Back
Top Bottom