Waziri Kamwelwe: Laini za simu zimeongezeka kutoka mil 39 mwaka 2015 hadi mil 43 mwaka 2020

Waziri Kamwelwe: Laini za simu zimeongezeka kutoka mil 39 mwaka 2015 hadi mil 43 mwaka 2020

Dam55

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
5,669
Reaction score
12,044
Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Eng Kamwelwe, ameliambia bunge kuwa matumizi ya simu za mikononi yameongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka ml 39 mwaka 2015 hadi ml 43 mwaka 2020.

Matumizi ya internet yameongezeka kutoka ml 9 mwaka 2015 hadi ml 25 mwaka 2020

Hilo pia limeenda sambamba na ufikishwaji wa huduma ya mawasiliano kwenye kata 703 zenye vijiji 2501 kwa jumla ya tsh Bil 118.

Aidha, serikali imejenga vituo 18 vya TEHAMA 10 vikiwa Zanzibar na 8 Tanzania bara.

Swali
Lain zilizo fungiwa zipo kwenye hii idadi?

Tanzania tuko nyuma sana kama taifa lenye watu ml 60 alafu matumizi ya Internet ni watu ml 25 tu hili bado ni tatizo.

Yaani kasi ya kukua kwa deni la taifa ni kubwa kuliko kasi ya ukuaji wa Technology ya mawasiliano.!!
 
Siokweli izodata nakama tupo mil 60 alafu 25 mil. wanatumia intranet basi tupo vizuri zaidi ya sana!! Karibia nusu wanatumia internet that's big thing kwa Afrika!!
Inabidi tubuni biashara kupitia upande huo sio kulaumu laumu tuu
 
Mkuu kwa upande wangu naona hii idadi bado ndogo sana.
 
Back
Top Bottom