A
Anonymous
Guest
Waziri Katambi, salama!
Naomba nikufikishie kilio cha sisi madereva wa Bajaj ambao tunatafuta riziki kwa kuendesha vyombo hivi. Kuna baadhi ya Watu wanaojiita “voice” ambao wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi maeneo tofauti ndani ya Dar es Salaam.
Tunapokuwa tunapakia abiria katika baadhi ya vituo, wanatukamata, wanachukua Bajaj zetu, wanafunga minyororo na kutulazimisha kulipa fedha wanazodai kuwa ni faini, mfano maeneo ya Mwenge, wakati mwingine wanafanya hadi vurugu na kuiba baadhi ya vifaa vya usafiri wetu.
Waziri, tunaomba msaada wako katika jambo hili. Kama kuna sheria, taratibu au mamlaka zinazotakiwa kusimamia vituo na magari ya abiria, tunaomba zifuatwe kupitia mamlaka husika, badala ya watu binafsi kuchukua sheria mkononi na kututoza fedha bila utaratibu unaoeleweka.
Sisi madereva tunategemea Bajaj hizi kwa ajili ya maisha yetu na familia zetu. Tunapofungiwa au kulazimishwa kutoa fedha, tunapata hasara kubwa na wakati mwingine tunashindwa hata kutimiza marejesho ya mikopo yetu.
Naomba Waziri ulifanyie kazi suala hili na ikiwezekana kuweka utaratibu wa wazi unaolinda haki za madereva na abiria, huku sheria ikiheshimiwa na kila upande.
Tunakuomba utusaidie sisi madereva wa bajaj. Mungu akubariki na akupe nguvu katika kutekeleza majukumu yako.
Dar es Salaam kila kituo wameweka viable usipakie wala kushusha hapa faini Sh 10,000.
Maeneo kama Big Brother, Mwenge pale Sheli ORYX Sheli na sehemu nyingi, hata Taksi Mtandao ukifuata abiria wanakupiga cheni hadi uwape hela.
Pia soma: LATRA wapiga marufuku mawakala kuwakamata bodaboda, Bajaj