Waziri Kenya aliwa kichwa na Uhuru kisa nzige

Waziri Kenya aliwa kichwa na Uhuru kisa nzige

Fiziolojia

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2019
Posts
815
Reaction score
1,080
Si mwingine bali ni Waziri wa Kilimo nchini Kenya, Mwangi Kiunjuri, ametumbuliwa na Rais Uhuru Kenyatta siku chache tu baada ya Kenya kuvamiwa na kundi kubwa la nzige ambao wanasemekana wametokea Kaskazini mwa nchi hiyo.

Inasemekana kilichomsababisha haswaa mpaka akatumbuliwa ni ile kauli yake aliyoitoa kwa umma kuwa endapo mtu yoyote ataona mdudu anayefanana nzige katika eneo lake alipo basi asisite kumpiga picha na kuituma kwenye mitandao ya kijamii ili serikali iweze kudhibitisha kama ni nzige au la.

Hali hiyo ilizusha sintofahamu nyingi katika mitandao ya kijamii katika nchi hiyo ambapo watu wengi walishangazwa na kauli hiyo ya Waziri Kiunjuri ambapo wengine walifikia hatua na kuamua kutuma picha za vituko na masihara katika mitandao yao ya kijamii.

IMG_20200114_232207.jpeg


IMG_20200114_231942.jpeg


IMG_20200114_225938.jpeg


IMG_20200114_231919.jpeg


IMG_20200114_232000.jpeg


IMG_20200114_232121.jpeg


IMG_20200114_232030.jpeg


IMG_20200114_232059.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • IMG_20200114_232000.jpeg
    IMG_20200114_232000.jpeg
    66.2 KB · Views: 1
Back
Top Bottom