Naomba nikupinge mkuu.
Hata hizo fukwe huwezi kushindana na maldives, indonesia, brazil, spain, hawaii etc kuna fukwe nzuri balaa, same kwa hayo matamasha yapo mengi kupita maelezo mazuri mara 100 kushinda ya znz.
Kinachotakiwa ni kutafuta vitu vya kipekee, vitu ambavyo havipatikani kokote duniani ila hapa kwetu tu.
Mfano Angalia thanda island, ipo Tanzania ila ni private island kubook tu kukaa hapo unatakiwa ufanye deposit ya dola $70,000 ambayo ni kama milioni 150, ni kisiwa cha kipekee miundo mbinu ya helicopter, wanyama kama tasa na vitu vyengine ambayo hupati kwengine.
Hii ni hulka yetu binadamu kinapotokea kitu ambacho hakipatikani kokote duniani basi tunamiminika ili na sisi tuonekano tumeshiriki.
Boresheni na tangazeni hivi vitu watu watakuja.