Waziri Kigwangalla aagiza kampuni ya Uwindaji ya OBC ya Loliondo kurudi walikotokea kabla ya Januari 2018

Ukiangalia report ni kwamba mpaka sasa wanasini mkataba wa miaka mitano mitano na sio 99 unaweza kusoma pia hapa
 
Mnyonyaji siku zote humnyonya mnyonge. Lakini wanyonge wakiungana na wakawa wa moja na wenye KAULI moja, Mnyonyaji hubadilika na kuwa mnyonge. UMOJA NI NGUVU. Hongera Mh. KIGWANGALA
 
Hiyo imekaa vizuri sana. Wazawa wameumizwa sana na kudhalilishwa katika ardhi yao. Tumwombe waziri afanikishe kuondoa unyonyaji huo na unyanyasaji uliokuwa wakifanyiwa wazawa kwa robo karne sasa katika eneo hilo.
Kila la kheri mhe. Waziri.
 
Kwanza tujiulize inakuwaje OBC wawe na ofisi mkabala na Ikulu pale Arusha? Ninavyofahamu maeneo karibu na Ikulu uwa ni ya serikali, na nyumba zilizo karibu na Ikulu nategemea watu wa usalama ama maafisa wa serikali wanapaswa kuishi. Sasa hawa OBC wana ofisi yao yaani mita chache tu kutoka kwenye geti la kuingia Ikulu ya Arusha. Nilifika ofisini kwao once; ila sijajua kama bado wapo pale.
 
Hongera sana Kigwangwala,I can now see light in the tunnel in this Ministry.It was in a mess.Ila usigeuke tena ukaanza kupokea rushwa.
 
hawa watu wamepata vibari kutoka kwenye serikali kufukuza tu na wana hati miliki sio kitu kidogo , tunarudi kwenye azimio la Arusha inavyoonekana
Ardhi ni mali ya wananchi chini ya udhamini wa Rais na akiona inafaa kwa manufaa mapana ya umma anaweza kuchukua ardhi yeyote nchini kwa madhumuni hayo na kwa kuzingatia sheria zilizopo.
 
Ardhi ni mali ya wananchi chini ya udhamini wa Rais na akiona inafaa kwa manufaa mapana ya umma anaweza kuchukua ardhi yeyote nchini kwa madhumuni hayo na kwa kuzingatia sheria zilizopo.
Ndiyo, lakini LAZIMA atoe compensation! Mgogoro utaweza kutokea endapo land and property valuations za serikali na OBC zitakapotofautiana!
 
Kuna watu wanatoa ushuhuda huku kuwa hao waarabu wameua ndugu zao wakati wewe unasema wamesaidia sana wananchi? Hapa nani mkweli?
 
Hao wanyonyaji ndio wanamiliki hicho chama anachotokea
 
Unakumbuka kete ya ewura kwa iptl? Pamoja na mikataba yao walinyimwa leseni ya ewula ya kuzalisha umeme wakaufyata! Subiri dawa ya waarabu ipo jikoni wananyimwa leseni ya kuwainda wanabakiza leseni ya kupiga selfie na fisi na nguruwe poli! [HASHTAG]#kigwangalathemessiah[/HASHTAG]
 
Mheshimiwa @Kigwangala.......usimsahau na huyu Green Miles......nadhani ujangili wake una ushahidi wa video kabisa........
 
Kuna watu wanatoa ushuhuda huku kuwa hao waarabu wameua ndugu zao wakati wewe unasema wamesaidia sana wananchi? Hapa nani mkweli?
Wacha uongo wameua wapi...waraabu wanakuja mwaka mara 4 to 10...na hawa ni very high profile sio kila mwarabu.
Wacheni chuki.

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Kama ukiingia hilo eneo mtandao unaandika karibu Uarabuni, na wameweka bendera yao wakati sio ubalozi. Kuna ushindi hapo kwa kufuata sheria za ardhi za nchi.

Hakuna fidia maana wenyewe ndio wame breach contract kwa kuweka kipande cha ardhi ndani ya nchi huru.
 
Kwa issue ya Loliondo acha iwe mbaya tu, waondokewe huyu mwekezaji siyo mwekezaji tu, watanzania wengi sana wameuwawa kwenye hicho kitalu chake.
 
Kwa issue ya Loliondo acha iwe mbaya tu, waondokewe huyu mwekezaji siyo mwekezaji tu, watanzania wengi sana wameuwawa kwenye hicho kitalu chake.
Za kuambiwa changanya na zako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…