Waziri Kigwangalla ataka utaratibu wa karantini kwa wageni uondolewe ili kuvutia Watalii

Kwahiyo Kigwangalla ameshakata tamaa Corona haitoisha!
Waingereza waliweka Lockdown 23 March 2020 wakiwa na wagonjwa 6650 vifo 336.
Leo hii wana Wagonjwa zaidi ya 210000 na vifo zaidi ya 31000. Ni wazi dunia haijajua namna ya kuukabili huu ugonjwa. Ipo haja ya kujifunza jinsi ya kuishi nao vinginevyo tutakifa na korona huku tunakufa Kwa njaa
 
Ili kulinda uchumi, nchi hii bhana
 
Hakuna mtu wa kuja. Wakati hata hamjielewi jinsi mnapambana.Ondoeni Karantini ila mjue hakuna mtu atakuja Tzee.
Yani hawaelewi kadri wanavyolegeza masharti ya Usalama ndivyo wageni nao wanapata hofu ya kuja nchini.. Hopeless
 
Naunga mkono hoja, pesa ni muhimu kuliko kitu chochote!.
P
P, nakuona huchelewi hata kidogo. Ila, mchemba zake alizichanga na kuzichanganua vilivyo. Mwenzetu zako sijui ka zinasikika vyema. Tatizo ni kuwa; sisi hatujafunga mipaka ila imejifunga yemnyewe. Mtalii huyo, Je, yupo hapa nchini au ndo atakuja ka miguu kupitia njia za pamya??
 
Kwa hili nasimama na Kigwangala.

Nashauri ile ndege yetu iliyoenda Madagascar ikurudi itue kwanza KIA ishushe box kadhaa pale ili mtalii akishuka anapewa kwanza chupa moja (welcome tibaCovid19) kisha ndio aruhusiwe kupokelewa na mwenyeji wake.
 
Watalii watakuja pale watakaposikia Watanzania wote wamechanjwa
 
Lugha na mapendekezo kama haya ndio uthibitisho kwa watu wa nje kuwa hatupigani vita dhidi ya corona.

Waziri anashindwa kutambua kuwa wageni hutoka sehemu tofauti tofauti na kama kila mtu anaingia tu, maana yake kila mtu ataweza kuwa ni hatari kwa mwenzake.

Nilitarajia aseme kila mgeni akifika atapimwa na akikutwa hata covid ataendelea na utalii wake. Nayo hii ingekwama kama mtalii ataamini kuwa watanzania katika maeneo atakayofika wanaweza kuwa na corona.

Kushindwa kutambua mambo kwa kiasi hiki ni tatizo kubwa sana. Naanza kuelewa kwanini hatutatoka hapa!!
 
Akauze vipuri na nyara za taifa. watapata fedha za kigeni, sio ndio anaitaka?
Bangi, mikonge ya tembo, nyani kasuku twiga...n.k vibali vya kuua ngedere, simba na hata kengewitu au kwamba hivi vitu haviuzwi nje?
 
Tobaaaa!
Hii inaitwa mauaji lojini...

Anyways juyisi za Madagascar zipo, tutagawiwa nyingi za misaada, nchi nzima..

Halahala maziko ya usiku mnene yasijirudie..

Everyday is Saturday........................... 😎
 
Dr. KIGWANGALA NI MBUNIFU. HII YOTE NIONAVYO MIMI BINAFSI, NI KTK KUTETEA MASLAHI YA WIZARA YAKE NA PATO LA TAIFA KIUJUMLA.

IKUMBUKWE YEYE AMERIDHIA KUBEBA DHAMANA KTK WIZARA ANAYOIONGOZA So ANA KILA SABABU YA KUIBUA MIKAKATI TIJA YA ENEO ANALO HUDUMU. MUACHENI ACHAPE KAZI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…