Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 651
- 433
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amepokea nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Finland nchini, Mhe. Anna Merrifield. Makabidhiano hayo yamefanyika Oktoba 13, 2026, katika Ofisi Ndogo za Wizara zilizopo Jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao baada ya makabidhiano, Mhe. Waziri Kombo amempongeza Balozi Merrifield kwa kuteuliwa kuwakilisha nchi yake nchini Tanzania. Aidha amemhakikishia ushirikiano wa karibu kutoka serikalini katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu yake ya kibalozi ili kuendeleza mahusiano mema yaliyopo.
Kwa upande wake, Mhe. Balozi Anna Merrifield ameshukuru kwa mapokezi mazuri na kuahidi kutoa ushirikiano thabiti wakati wote wa utumishi wake. Ameeleza dhamira yake ya kuendeleza na kukuza zaidi uhusiano wa kidiplomasia pamoja na ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya nchi hizo mbili