Waziri Kombo apokea nakala za hati za utambulisho za Balozi Mteule wa Finland

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amepokea nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Finland nchini, Mhe. Anna Merrifield. Makabidhiano hayo yamefanyika Oktoba 13, 2026, katika Ofisi Ndogo za Wizara zilizopo Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao baada ya makabidhiano, Mhe. Waziri Kombo amempongeza Balozi Merrifield kwa kuteuliwa kuwakilisha nchi yake nchini Tanzania. Aidha amemhakikishia ushirikiano wa karibu kutoka serikalini katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu yake ya kibalozi ili kuendeleza mahusiano mema yaliyopo.

Kwa upande wake, Mhe. Balozi Anna Merrifield ameshukuru kwa mapokezi mazuri na kuahidi kutoa ushirikiano thabiti wakati wote wa utumishi wake. Ameeleza dhamira yake ya kuendeleza na kukuza zaidi uhusiano wa kidiplomasia pamoja na ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya nchi hizo mbili









​
 

Attachments

  • IMG-20261015-WA0077.jpg
    66.7 KB · Views: 6
  • IMG-20261015-WA0076.jpg
    51.4 KB · Views: 5
  • IMG-20261015-WA0085.jpg
    81.2 KB · Views: 6
  • IMG-20261015-WA0079.jpg
    53 KB · Views: 5
  • IMG-20261015-WA0083.jpg
    90.7 KB · Views: 6
  • IMG-20261015-WA0086.jpg
    94.8 KB · Views: 3
  • publer-1792037417255.mp4
    4.6 MB
Safiii Mhe Kombo wa Tanzania tunaitaji kusonga mbele kwa mbele
Kupitia Marafiki wa kweli Kombo ukweli ni mtu na nusu yule ni Mwamba kweli kweli ✍️
 
Your browser is not able to display this video.
 
Wenye Wivu poleni tu muhimu kwenu kwetu Taifa lisonge mbelembele✍️
 
Tanzania yenye Amani inapendeza sana
Viongozi wa Kitaifa wapo kupokea wageni wakubwa wenye hadhi ya Ma Balozi

Wkt na Chadema wapo kutumiza mipango yao kwanjia ya Tozo jamii ya Tone tone!!!

Mwisho tunajivunia Amani kwa pamoja yenye kuleta fursa mbali mbali

tunampongeza kiongozi wetu mwenye Subra sana mwenye kuipenda nchi yake

mwenye kutupenda Wananchi wake na mwenye kupenda Amani

RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN

Tutakulinda kwa wivu mkubwa na tutakuombea usiku na Mchana Mungu mkuu akulinde wewe na Wasaidizi wako wema✍️
 
Nani kama MAMA hakuna kwanini tusijivunie MAMA yetu Taifa limebarikiwa Viongozi wenye Hekima watulivu sana ✍️
 
MUNGU MKUU atunusuru na El Nino Watanzania wote ✍️
 
Kwani
Mama lenu Leo limeenda wapi?
 
well done waziri Kombo 🤝
 
MUNGU MKUU atunusuru na El Nino Watanzania wote ✍️
Ni kama kwenye hii habari unajistukia ndio maana unapost ww tu. Juzi rais kapokea nyaraka za Balozi mwingine, kwanini huyu sio yeye bali Kombo?
 
kombo anapokea mabeberu ndio maana nchi yetu imeuzwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…