Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
WAZIRI KOMBO APOKEA TAARIFA YA KAMATI MAALUM YA MAPITIO YA KITUO CHA DKT. SALIM AHMED SALIM
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo, (Mb), amepokea Taarifa ya Kamati Maalum ya Wizara kuhusu mapitio ya kituo cha uhusiano wa kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim cha Jijini Dar es Salaam. iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Balozi Khamis Sued Kagasheki.
Katika Taarifa hiyo, Balozi Kagasheki aliwasilisha matokeo ya uchambuzi uliofanywa na Kamati na kuainisha mapungufu yaliyobainika kwenye maeneo mbalimbali na kutoa mapendekezo husika kuboresha Kituo hicho ili kikidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye katika nyanja za diplomasia na uhusiano wa Kimataifa.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo Mhe. Waziri Kombo aliishukuru Kamati hiyo kwa ufanisi, uzalendo,taaluma, ukweli na uwazi katika kutekeleza jukumu ililopewa.
Mhe Waziri alibainisha kuwa mapendekzo ya Kamati yatachangia kuboresha Kituo hicho na hivyo kufikia malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanadiplomasia Namba Moja Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukifanya Kituo hicho kuwa kituo cha umahiri,
fikra na rejea katika kukuza wanadipolomasia wa Tanzania ili waweze kutoa mchango unaotarajiwa katika nyanja ya diplomasia na uhusiano wa kimataifa nchini na ukanda wa Afrika.
Mhe. Waziri pia aliainisha utayari wa Wizara katika kutekeleza mapendekezo ya Kamati ili kukifanya Kituo hicho kiakisi taswira na kuenzi kazi na mchango mkubwa wa Mwanadiplomasia Nguli nchini Balozi Dkt. Salim Ahmed Salim alizofanya na kuutoa katika diplomasia ya Tanzania, Bara la Afrika, Umoja wa Mataifa na ulimwenguni kwa ujumla.
Balozi Kombo aliwahakikishia wajumbe wa Kamati hiyo kuwa, Wizara chini ya uongozi wake itaandaa mpango kazi wa kutekeleza mapendekezo yao kwa kuaza na maandalizi ya Mfumo wa Kisheria ambao utakamilika mapema ili kuleta mageuzi ya kweli.