Waziri Kombo ashiriki hafla ya maadhimisho ya Siku ya Taifa la UAE

Waziri Kombo ashiriki hafla ya maadhimisho ya Siku ya Taifa la UAE

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo ameshiriki hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Taifa la UAE iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya UAE akiwa ni Mgeni wa Heshima.

Hafla hiyo imefanyika mjini Abu Dhabi tarehe 05 Desemba, 2024 ambapo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE Mheshimiwa Sheikh Abdullah bin Zayed bin Sultan Al Nahyan alikuwa Mgeni Rasmi.

Washiriki wengine walikuwa ni wanadiplomasia walioko nchini UAE na viongozi wengine wa Serikali ya UAE.

Katika hafla hiyo Balozi Kombo alikutana na kusalimiana na Mheshimiwa Sheikh Abdullah Al Nahyan , Mhe Makhboot na Mhe Reem Al Hashimy pamoja na viongozi wengine wa Serikali ya UAE.

IMG-20241206-WA0023.jpg

Mhe. Kombo pia alikutana na kusalimiana na mabalozi wa nchi za Afrika na kuwapongeza kwa mshikamano wanaoundeleza kama wa Jumuiya hususan nchi za SADC ambapo hivi karibuni wamefanya hafla ya makabidhiano ya Uenyekiti kutoka kwa Balozi wa Angola kwenda kwa Balozi wa Zimbabwe.

Tarehe 02 Desemba, 2024 UAE iliadhimisha miaka 53 ya Umoja wao tangu ulipoasisiwa mwaka 1971.

IMG-20241206-WA0024.jpg
IMG-20241206-WA0027.jpg
IMG-20241206-WA0028.jpg
IMG-20241206-WA0030.jpg
IMG-20241206-WA0031.jpg
 

Attachments

  • IMG-20241206-WA0025.jpg
    IMG-20241206-WA0025.jpg
    147.1 KB · Views: 3
  • IMG-20241206-WA0026.jpg
    IMG-20241206-WA0026.jpg
    677 KB · Views: 5
  • IMG-20241206-WA0029.jpg
    IMG-20241206-WA0029.jpg
    93.1 KB · Views: 6
  • IMG-20241206-WA0032.jpg
    IMG-20241206-WA0032.jpg
    114.1 KB · Views: 3
  • IMG-20241206-WA0033.jpg
    IMG-20241206-WA0033.jpg
    148.3 KB · Views: 4
Back
Top Bottom