Waziri Kombo na ujumbe wa wafanyabiashara wa Sweden, asisitiza ushirika

Waziri Kombo na ujumbe wa wafanyabiashara wa Sweden, asisitiza ushirika

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
๐—ช๐—”๐—ญ๐—œ๐—ฅ๐—œ ๐—ž๐—ข๐— ๐—•๐—ข ๐—”๐—ž๐—จ๐—ง๐—”๐—ก๐—” ๐—ก๐—” ๐—จ๐—๐—จ๐— ๐—•๐—˜ ๐—ช๐—” ๐—ช๐—”๐—™๐—”๐—ก๐—ฌ๐—”๐—•๐—œ๐—”๐—ฆ๐—›๐—”๐—ฅ๐—” ๐—ช๐—” ๐—ฆ๐—ช๐—˜๐——๐—˜๐—ก, ๐—”๐—ฆ๐—œ๐—ฆ๐—œ๐—ง๐—œ๐—ญ๐—” ๐—จ๐—ฆ๐—›๐—œ๐—ฅ๐—œ๐—ž๐—œ๐—”๐—ก๐—ข ๐—ช๐—” ๐—•๐—œ๐—”๐—ฆ๐—›๐—”๐—ฅ๐—” ๐—ก๐—” ๐—จ๐—ช๐—˜๐—ž๐—˜๐—ญ๐—”๐—๐—œ

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Sweden, ukiongozwa na Rais wa Chemba ya Biashara ya Swedenโ€“Africa, Bi. ร…sa Jarskog, leo tarehe 14 Oktoba 2026 jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Kombo amesisitiza dhamira ya Serikali ya Tanzania ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na Sweden, hususan katika kukuza biashara, kuvutia uwekezaji na kuendeleza ushirikiano kati ya sekta binafsi za nchi hizo mbili.

Mhe. Kombo ameeleza kuwa Tanzania inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa uwekezaji katika sekta za kimkakati, zikiwemo nishati, miundombinu, maji na usafi wa mazingira, teknolojia, madini na viwanda. Aidha, amepongeza ujio wa kampuni za Sweden zikiwemo Linjemontage, Buenco, ECOLOGO, Metrum, PrismaTibro na Siemens Energy, ambazo zinawakilisha maeneo mbalimbali ya teknolojia na huduma muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa Tanzania.

Kwa upande wao, Rais wa Chemba ya Biashara ya Swedenโ€“Africa, Bi. ร…sa Jarskog, pamoja na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Ingrid Johansson, wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mapokezi mazuri na ushirikiano uliowezesha kufanyika kwa ziara hiyo. Wameeleza kuwa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Sweden wamevutiwa na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania na wana matarajio makubwa ya kuanzisha miradi ya uwekezaji na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

Katika kuendeleza ziara hiyo, ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Sweden unatarajiwa pia kutembelea Dodoma na Zanzibar kwa lengo la kutambua fursa zaidi za biashara na uwekezaji, pamoja na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali ili kuweka misingi ya ushirikiano wa kiuchumi na utekelezaji wa miradi ya uwekezaji katika maeneo hayo.
publer-1792039096629.jpg
publer-1792039061344.jpg
publer-1792039104004.jpg
publer-1792039100188.jpg
publer-1792039075312.jpg
publer-1792039080133.jpg
publer-1792039106524.jpg
publer-1792039093110.jpg
publer-1792039066916.jpg
publer-1792039071775.jpg
publer-1792039088564.jpg
publer-1792039084942.jpg
publer-1792039112459.jpg
publer-1792039115299.jpg
publer-1792039109761.jpg
publer-1792039125122.jpg
publer-1792039122296.jpg
publer-1792039118882.jpg
 
Back
Top Bottom