Pre GE2025 Waziri Lukuvi aitaka Ofisi ya Waziri Mkuu kuanzisha Daftari la "Faida Za Samia" kila eneo nchini

Pre GE2025 Waziri Lukuvi aitaka Ofisi ya Waziri Mkuu kuanzisha Daftari la "Faida Za Samia" kila eneo nchini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakuu,

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu William Lukuvi ameitaka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu kuandaa Daftari la Faida litakaloonesha kazi na shughuli za Serikali zilizofanyika katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kabla ya Oktoba 2025, kipindi cha uchaguzi mkuu.


Akizungumza na watendaji wa ofisi hiyo leo Machi 14, 2025 Jijini Dodoma, Waziri Lukuvi amewataka kutumia ubunifu na kila njia kuhakikisha taarifa za utekelezaji wa miradi na mafanikio ya Serikali katika kila eneo la nchi zinasema na kusikika kwa wananchi wote kwa kuwa ni haki ya wananchi kufahamu Serikali yao imefanya nini.

“Sasa wananchi wale tunatarajia watamuunga mkono Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi ambazo amezifanya katika kipindi chake cha uongozi…hiki kipimdi cha kwanza lakini wananchi watazijuaje?. Nafahamu wanajua kwa kuwa kazi hizi zimefanyika kila mahali vijijini wiliayani na mikoani lakini sisi ofisi ya waziri Mkuu tunalojukumu la kuziunganisha hizo kazi na kuwaambia wananchi kwa uhakika”. amesema Waziri Lukuvi
Wasisahau pia hili kuweka humo
 
Ukisoma riwaya ya Shaaban Robert ‘Kusadikika’ utagundua kuwa alikuwa nabii wa kweli. Alitabiri Tz ya leo miała hiyo ya 60. Kweli nchi yetu imepatwa. Ole wao vizazi vijavyo kama hatutazinduka na kubadilika
 
Lukuvi na Majaliwa ni wakati wao wa kuachia nafasi vijana

Waoga sana maisha mitaani kwa nini wakati wana mafao kibao miaka nenda rudi

Mama Samia nanshukuru kwenye succession plan kumuweka Nchimbi

Hivi vikongwe ni muda kuwa phased out

Mama Samia spearhead zoezi la ku phase out hivi vizee visivyoamini kuwa vijana chini ya age yao wanaweza

Tusaidie tafadhali ku vi phase out

Nchi haiwezi kuwa kila wakati inategenea vikongwe tu ambavyo havina mpango wa succession plan kwenye majimbo yao au kuwa tayari kuwa phased out

Lukuvi na Majaliwa phase out Mheshimiwa mwenyekiti hao kwa hiari yao hawana mpango wa kutoka

Make a very bold decision to phase them out
Unaujua umri wa huyo unayemtaka awaondoe hao ulowataja? Vipi makamu mwenyekiti? Nchimbi ndiye anawakilisha kundi la vijana sio?
 
Unaujua umri wa huyo unayemtaka awaondoe hao ulowataja? Vipi makamu mwenyekiti? Nchimbi ndiye anawakilisha kundi la vijana sio?
Nchimbi ni generation ya pili ya uongozi
Hao wengine ni generation ya kwanza ya Nyerere

Generation ya kwanza hiyo ya Nyerere waondoke ndio maana nasema uchaguzi ujao wengi wawe age ya nchimbi na chini ya hapo

Nchi kubadilika ni.kubadili uongozi ki.umri pia
 
Katika kipindi cha utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Lukuvi anataka kuhakikisha kwamba wananchi wanapata taarifa sahihi na wazi kuhusu mafanikio na faida zinazotokana na sera na miradi ya serikali.

Hii ni hatua muhimu katika kuwajengea wananchi uelewa kuhusu maendeleo yanayoendelea nchini.

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba wakati wa utawala wa Rais John Magufuli, wazo kama hili lilikuwa gumu kutekelezwa.

Lukuvi anapaswa kueleza kwa uwazi ni kwa nini alishindwa kuwasilisha pendekezo kama hili wakati wa utawala wa Magufuli. Je, ni kwa sababu ya mazingira ya kisiasa au kutokuwepo na mfumo mzuri wa kuwasilisha taarifa?

Hii ni muhimu ili kuelewa tofauti ya mtazamo kati ya utawala wa Magufuli na wa Samia.

Katika kipindi cha Magufuli, kulikuwa na miradi kadhaa mikubwa ya kimkakati, kama vile ujenzi wa barabara, reli, Rada,viwanja vya ndege,Barabara za juu, kuondoa vyeti fake,kuzuia safari za nje ya nchi, kutumbua watumishi na haswa mawaziri,wakuu wa taasisi, na watumishi hewa, na miradi ya umeme.

Hata hivyo, baadhi ya wananchi waliona kuwa hawakupata faida moja kwa moja kutokana na miradi hii. Wengi walihisi kwamba taarifa kuhusu maendeleo haya hayakutolewa kwa uwazi, na hivyo kuleta hisia za kutokukubaliana na serikali.

Hali hii inaweza kuwa sababu ya Waziri Lukuvi kutaka kuanzisha daftari hili la "Faida za Samia" ili kujenga uhusiano mzuri kati ya serikali na wananchi.

Kwa upande mwingine, faida za utawala wa Samia zimeanza kuonekana katika sekta mbalimbali. Rais Samia ameweka msisitizo katika kuboresha huduma za afya, elimu, na kuwezesha wanawake kiuchumi.

Hizi ni hatua zinazoweza kuonekana moja kwa moja na kutoa faida kwa wananchi, tofauti na wakati wa Magufuli ambapo baadhi ya miradi ilionekana kama ya kitaifa zaidi bila kuhusisha jamii moja kwa moja.

Kwa hivyo, ni muhimu kufafanua tofauti hizi. Katika utawala wa Magufuli, baadhi ya miradi ililenga zaidi katika kujenga miundombinu na kutekeleza sera za maendeleo, lakini wananchi walihisi kuwa hawakuwa sehemu ya mchakato huo.

Kwa upande wa Samia, kuna juhudi za kuhusisha wananchi katika maamuzi na kuwapa nafasi ya kushiriki katika maendeleo ya jamii zao.

Wazo la Waziri Lukuvi pia linaweza kuunganishwa na hilo la uwazi na uwajibikaji. Katika dunia ya leo, wananchi wanahitaji taarifa sahihi kuhusu wanavyoweza kunufaika na miradi ya serikali. Daftari la "Faida za Samia"

litatoa fursa kwa wananchi kujifunza kuhusu miradi mbalimbali na jinsi wanavyoweza kuhusika katika kufanikisha malengo ya serikali.

Ni muhimu pia kutambua kwamba mabadiliko haya yanaweza kuleta changamoto. Kunaweza kuwa na upinzani kutoka kwa wale ambao wanaona daftari hili kama njia ya kisiasa ya kutangaza mafanikio ya serikali.

Hata hivyo, ikiwa itatekelezwa kwa uwazi na kwa lengo la kutoa taarifa sahihi, inaweza kuwa chombo muhimu katika kuimarisha uhusiano kati ya serikali na wananchi.

Kwa kumalizia, ni wazi kwamba Waziri Lukuvi ana matumaini makubwa kuhusu kuanzishwa kwa Daftari la "Faida za Samia."

Hata hivyo, ni muhimu kwa viongozi wa serikali kuzingatia mafunzo yaliyopatikana kutoka utawala wa Magufuli. Wanapaswa kuelewa kuwa uwazi na ushirikishwaji wa wananchi ni muhimu katika kujenga imani na kutoa fursa kwa kila mtu kunufaika na maendeleo.

Kila utawala unapaswa kujifunza kutokana na historia ili kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora kwa wananchi na kuleta maendeleo endelevu.
 
Hii inamaanisha kuwa wananchi wamekuwa kama nguruwe pori kuwa hawaishi kwenye hayo maeneo hadi waanze kupigiwa kelele kuhusiana na yaliyofanyika?
Viongozi wetu wazeni basi mambo chanya dhidi ya wananchi wenu siyo hayo ujinga ujinga.

Badala ya kusema wafanyakazi wa ofisi yake wachukue madaftari na kuyarekodi yote ambayo hayajafanywa na Serikali ya Samia kutoka kwa wananchi ili yatatuliwe yeye anawaza kupewa sifa za uongo.
 
Back
Top Bottom