Waziri Lukuvi tembelea maeneo ya Dar es Salaam, kuna viwanja vingi havijaendelezwa

Tumefatilia sana mdau, Tatizo ni kwamba huyo masawe anatumia sana Polisi kutisha wananchi wanapotaka kuchonga hiyo barabara, pia anatumia baadhi ya watu Idara ya ardhi ofisi ya Halmashauri Wilaya ya Ilala kupotosha hilo jambo ili hiyo barabara ionekane haina maana kwa wananchi.

Pia huyo masawe anataka kuweka zuio mahakamani kutaka kuzuia hiyo barabara isichongwe na anafanya makusudi kutaka kuweka zuio ili akamilishe mipango yake ya kuuza hilo eneo.

Hilo eneo ni zaidi ya ekari tano lipo katikati ya Makazi ya watu eneo la Kinyerezi pia ni pori kubwa ambalo uhalifu unafanyika usiku wananchi wanaporwa vitu vyao, wezi wanajificha. Imefika hatua wezi wanaiba mifugo maeneo mengine halafu wanakuja kuchinjia kwenye hilo eneo, wananchi tunakuta kwato, vichwa na ngozi za mifugo asubuhi.

Ndio maana tunaomba serikali kuu kupitia Wizara ya Ardhi watusaidie kupata hiyo barabara sababu wananchi hatuna barabara ya kupita pia wamshauri huyo masawe aendeleze hilo eneo ili kuepusha uhalifu katika hilo eneo sababu sasa ni zaidi ya miaka 15 tangu ameanza kulimiliki hilo eneo huyo masawe.

Tunaomba Mh Waziri Lukuvi pia Mh Rais Magufuli waweze kutusaidia katika hili jambo sababu baadhi ya watendaji kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ilala sio waaminifu kwa kua wanamsaidia huyo masawe.
 
Hiki ulichokieleza hapa ndio uhalisia wa maeneo yote hawa jamaa wana mapori makubwa hata barabara kutoa hawataki.
Hili tatizo ni kubwa mno.
 
Mipango miji wa halmashauri?
 
Hiki ulichokieleza hapa ndio uhalisia wa maeneo yote hawa jamaa wana mapori makubwa hata barabara kutoa hawataki.
Hili tatizo ni kubwa mno.
Ni tatizo kubwa hasa,
Huyo masawe yeye haishi huo mtaa ila ameshikilia hilo eneo ekari tano zaidi ya miaka 15 bila kuliendeleza na lipo katikati ya Makazi ya watu.
Kitu kibaya zaidi ni kwamba anazuia hata barabara halali ambayo imepimwa na serikali inatambua katika huo mtaa, hivyo hadi sasa wananchi wanapata tabu sana kwa kua hamna barabara.

Hivyo tunaomba Mh Raisi Magufuli na Wizara ya ardhi watusaidie hilo tatizo pale Tabata Kinyerezi.
 
Mipango miji wa halmashauri?
πŸ™‚ hao hao mkuu πŸ˜€
Na wengine wapo mitaani registered planners au Fika TPRB (Bodi ya usajili wa Planners watakupa mtu sahihi awasaidie)
 
Tatizo hawa viongozi wa serikali za mtaa hawajui chochote kuhusu sharia ya ardhi pia waoga na wengi maisha magumu

πŸ™‚ hao hao mkuu πŸ˜€
Na wengine wapo mitaani registered planners au Fika TPRB (Bodi ya usajili wa Planners watakupa mtu sahihi awasaidie)
Sawa
 
Huyo anavuna kupitia Watu wanaoendeleza wanaomzunguka.

Hao wanaojenga ndio wanaoongeza thamani, ndio wanaoongeza idadi ya Watu na kuboresha na yeye anaoona thamani inapanda kwa eneo lake.

Hivyo yeye anawaibia ninyi. Maana hashiriki kuboresha ila anafurahia faida..na tena haimtoshi anaendelea kutaka kupata zaidi!? Mwizi huyo wa juhudi za umma.

Andikeni kuomba eneo hilo litwaliwe na manispaa kwa matumizi ya huduma za kijamii. Na kumuandikia na Rais kumuomba itwaliwe kwa maslahi ya mtaa.. zahanati, shule ya awali, msingi, secondary... Halafu mnaazimia kuanzia vikao vya mtaa kama shamba pori ...
 
Tatizo hawa viongozi wa serikali za mtaa hawajui chochote kuhusu sharia ya ardhi pia waoga na wengi maisha magumu



Sawa
Kisheria serikali za mitaa hawana mamlaka ya kutatua migogoro ya Viwanja ambavyo vimeshapimwa na vina Hati,

Jukumu la kutatua matatizo ya Viwanja vilivyopimwa ni la Halmashauri husika na serikali kuu.

Hivyo huyo masawe anatumia baadhi ya watumishi Idara ya Ardhi, Halmashauri ya Wilaya ya Ilala ili kuzuia hiyo barabara ambayo ipo katika Viwanja vilivyopimwa hapo tabata Kinyerezi ishindwe kuchongwa kwa maslahi yake binafsi.
Wananchi wanapata tabu, serikali haichukui hatua yeyote dhidi ya huyo masawe.

Pia huyo masawe analaumiwa na wananchi wengine maeneo ya Kifuru na Hapo Kinyerezi kwa kuzulumu maeneo yao, anatumia Polisi kutisha na baadhi ya watumishi Idara ya ardhi Halmashauri Wilaya ya Ilala kuzulumu haki za wananchi.
 
Wazo zuri sana mdau, Kinyerezi ni mji mkubwa, wakisasa na ulishaendelea ila huyo masawe ndio anamiliki hilo pori ekari tano katikati ya mji,
Kwa jeuri ya Cheo chake pale Tanroads na pesa zake ndio anafanya hivyo vituko vya kufunga barabara halali iliyopimwa na kuthibitishwa na serikali,

Pia katika hilo eneo ekari tano Kuna uhalifu mkubwa unafanyika usiku.

Kitu kingine cha kushangaza ni kwamba huyo masawe ana Cheo kikubwa sana Tanroads na anafahamu Sheria za barabara ambayo imeshapimwa ila anajitapa na kufanya makusudi kwamba hata hicho Cheo hapo Tanroads kapewa na Mh Rais Magufuli hivyo hakuna mtu wa kumfanya chochote.

Mh Rais Magufuli tunakuomba mfatilie huyo masawe, binafsi sina hakika Mh Rais akawa na mafungamano na mtu kama huyo masawe anaezulumu maeneo wananchi huko Kinyerezi, Kifuru n.k imefika hatua anazuia barabara halali iliyopimwa na kuthibitishwa na serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…