Tetesi: Waziri Maghembe kutumbuliwa

Katika watu waliokuwa hawaamini ushirikina basi ni mimi. Kwa jinsi huyo Maghembe alivyoanza kuitwa mzigo na jinsi akiongea hana mvuto, lakini bado ni mbunge na uwaziri juu, hapo nimechoka kabisa. Cha ajabu huyo Waziri mkuu anashughulikia hilo suala mwenyewe wakati dalilizote za uongo ziko wazi. Saa hii huyo mzee anapiga ramli tu ili asifukuzwe uwaziri.
 
Nauliza hiviiiiiiiiii eti ile mahakama ya mafisadi ipo au haipo ? Kama ipo kwanini hawa wasipelekwe huko ?
 
ningekua ni mimi, waziri mkuu anakuja kwa wizara yangu, anagundua chezo, siwezi kubaki, ona sas anakua bubu
 
Alinifukuza chuo huyu akafanya nihamie bara lingine kabisa . Naamini zamu yake nae imefika kuishi kama shetani.

[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG].

Mkuu bily alikuchezesha sebene nini?

Sijaelewa hata kidogo hapo...
 
Mkuu sio kweli kwamba waziri mkuu hawezi kusema uongo.
Hadi ataje kabisa na kiasi cha pesa ambacho John aliuzwa unadhani aliropoka eeh? Kama ni kuropoka kwanini hajakisia bei lakini akataja bei halisi? We subiri uone huyo waziri na majangili wenzake jinsi watakavyopukutishwa kutoka kwenye nafasi zao.

[HASHTAG]#bringbackourrhinoalive[/HASHTAG]
 
Wewe umejuaje kama hicho kiasi kilichotajwa ni halisi?
 
Huyo faru alipotea lini?
 
Waziri Mkuu hawezi sema uongo?? Hebu acha kutulaghai, PM ni binadamu kama binadamu wengine. Anaweza potoshwa na wasaidizi wake pia. Tuiache tume ilioteuliwa na PM ifanye kazi
 
Ishu ya kusemwa ukweli au uongo siyo ishu sana ishu kifo cha faru ndo utata,kuna dalili zote kuwa alipigwa dili sasa kuthibitisha hilo ndo ngumu kidogo ila pia pm anataka kumshika mchawi wake kitu ambacho kina kuwa ngumu now kwani kaburi la faru halipo labda atumie mbinu nyingine ila pia kama aliuzwa na pm anajua aliko akamchukue ili amalizane nao vizuri sahani moja.
 
Acheni kuhukumu bila ya kujua undani wa suala lenyewe. Hivi leo kipindi cha Star Television cha Tuongee Asubuhi kilikuwa na Mada isomekayo Sintofahamu ya sakata la Faru John. Katika kipindi hicho waongoza mada wa Mwanza na Dar es Salaam pamoja na wachambuzi wao walitumia muda mrefu wakimtaka Waziri Maghembe ajiuzulu; Kwa maoni yangu naona hii sio kumtendea haki Waziri huyo bila ya kujua undani wa suala lenyewe; Je, kama Waziri Maghembe ndio alimpa taarifa mkuu wake wa kazi yaani Waziri Mkuu alishughulikie kutokana na wahusika/Mhusika mkuu wa ufisadi wa Faru huyo ni wale wasiogusika (Untouchable?) hivyo akaona ni vyema suala hilo lianzie kwa PM? Si tulishasikia lile sakata la pembe za ndovu zilizotolewa taarifa na mwandishi nguli kutoka Uingereza kwamba majangili wakubwa wa pembe za ndovu ni watu maarufu nchini. Sasa kwa nini tunamhukumu Maghembe?
 
Ni ile ile ohhhhh, ni ile ile., akitumbuliwa atapangiwa kazi nyingine.
 
Magufuli aanze kuwaamini na wapinzani awateuwe nao.. Maana Ccm ni ukoo wa panya..
Magufuli ni mtu wa visasi...kamwe hawezi kuwateua wapinzani zaidi ya alivyompoza Mrema kwa jitihada zake za kubomoa upinzani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…