Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alikufukuza wap mkuu
Haswa ukitumia Sakata la Richmond kama 'case study !Mkuu sio kweli kwamba waziri mkuu hawezi kusema uongo.
Kama waziri maghembe anashindwa kusimamia rasilimali zetu, na wakati huohuo akishirikiana na majangili, hadi aje waziri mkuu kuna haja gani yeye kuwepo kwenye nafasi yake?Acheni kuhukumu bila ya kujua undani wa suala lenyewe. Hivi leo kipindi cha Star Television cha Tuongee Asubuhi kilikuwa na Mada isomekayo Sintofahamu ya sakata la Faru John. Katika kipindi hicho waongoza mada wa Mwanza na Dar es Salaam pamoja na wachambuzi wao walitumia muda mrefu wakimtaka Waziri Maghembe ajiuzulu; Kwa maoni yangu naona hii sio kumtendea haki Waziri huyo bila ya kujua undani wa suala lenyewe; Je, kama Waziri Maghembe ndio alimpa taarifa mkuu wake wa kazi yaani Waziri Mkuu alishughulikie kutokana na wahusika/Mhusika mkuu wa ufisadi wa Faru huyo ni wale wasiogusika (Untouchable?) hivyo akaona ni vyema suala hilo lianzie kwa PM? Si tulishasikia lile sakata la pembe za ndovu zilizotolewa taarifa na mwandishi nguli kutoka Uingereza kwamba majangili wakubwa wa pembe za ndovu ni watu maarufu nchini. Sasa kwa nini tunamhukumu Maghembe?
Hata mimi nimeshangaa.......Mkuu sio kweli kwamba waziri mkuu hawezi kusema uongo.
Kuna watu wapowapo tu kama Mazombie...Ndio maana mnyama yeyote akipata matatizo lazima Magembe kama waziri apewe taarifa na yeye ndio wa mwisho kuizinisha na kutoa tamko hiyo ndio kazi yake.
Huna Elimu ya juu
Go back to school Dude.
swissme
Mmhhh...Hiyo wizara ni ngumu, vinginevyo apewe Makonda au Gumbo.
Usihukumu cinema ifike mwisho. Ila tu lazima tuseme ukweli, watu kama Prof. Maghembe wanapaswa kukaa nyumbani na kubaki kuwa washauri wa vijana. Mzee kama huyu ameshalichangia taifa vya kutosha, kama haikutosha haiwezi kutosha tena saa hii. Kasi hii ya sasa awaachie akina Makonda tu waende nayo maana akina Prof. Maghembe ni sehemu ya hali hii tuliyonayo kama taifa ambayo Rais Magufuli inamhangaisha hivi sasa.Kuna kila dalili kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amekalia kuti kavu, tena kavu kwelikweli.
Sakata la kuuzwa kwa faru John na kisha yeye kubariki uuzwaji huo ni udhaifu mkubwa sana na kigezo tosha cha kumfanya aondolewe kwenye nafasi yake ya sasa. Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa, inasemekana faru huyo aliuzwa kwa thamani ya Tsh milion 200, ambapo wauzaji walitanguliziwa malipo ya Tsh milioni 100. Waziri mkuu hawezi kusema uongo. Ni dhahiri anazo taarifa za uhakika za kiintelejensia kwamba faru ameuzwa kwa bei hiyo ya kutupwa. Ndio maana wahifadhi wanashindwa kuonyesha kaburi lake lilipo kama kweli mnyama huyo wa porini alikufa.
Sintofahamu hii inakolezwa zaidi na Maghembe mwenyewe aliyediriki kumdanganya Waziri Mkuu, kwa kushirikiana na wezi wenzake, kwamba faru yule 'amekufa' huku akijua kwamba anasema uongo. Kwa sababu hizi, pamoja na sababu nyingine ambazo bado hazijawekwa wazi ili kumtumzia heshima profesa huyu, kuna kila dalili kwamba huenda Rais, Dr Joseph Pombe akatengua uteuzi wake kabla hajamaliza faru wetu.
Ikiwa waziri mwenye dhamana ya kulinda rasilimali zetu, ama kwa kujua au kwa makusudi, ameamua kushirikiana na majangili kufilisi rasilimali zetu kuna haja gani ya kuendelea kukalia kiti cha uwaziri? Kwa dhati kabisa bila unafiki wowote, mimi namuunga Rais Pombe katika utumbuaji huu. Ifike wakati kila mtu aheshimu rasilimali za taifa kwa manufaa ya watanzania wa sasa na vizazi vijavyo.
Mungu mbariki Rais wetu, Mungu wabariki watanzania, Mungu bariki rasilimali zetu za Taifa. Amen.
Ndiyo watu wanaoaminiwa na Mhe.Mmhhh...
OVA
Inategemea Rais alizungumzia dawa za kipindi gani na waziri mkuu alizungumzia dawa za kipindi ganiWazir mkuu alisema kuwa serikali imetoa trilion 1 kununua madawa. Magufuli akasema serikali imetoa billion 200 kunuNua dawa. Nani apo ni muongo?