Kwa mtazamo wangu nadhani hii ina nafuu.Darasa la kwanza na la pili mkazo utakuwa Kusoma Kuandika na Kuhesabu (KKK)
Na asipofaulu tena, je?
Michezo inakuwepo ila haiwi kama sehemu ya somo ambalo lina alama bali kwa ajili ya kuwafanya wasiwe "bored".
Duh! Ndo maana tunakosa hata watu wa kupeleka olimpiki?
Kwenye shule za wenzetu wametenga siku moja kwa wiki maalum kwa michezo tuu.
Mkuu michezo haitafutwa kabisa. Bado itakuwepo ila kwa maana ya recreation na kuibua vipaji pia.Katika yote hao watoto lazima wajue kusoma, kuandika na kuhesabu kwanza!
Mkuu kuna umuhimu wa wanafunzi kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.
Lakini pia tusisahahu kuwa watoto nao wana vipaji mbali mbali ambavyo vikiendelelezwa wakiwa bado wadogo wanaweza kuwa na potential kubwa kwenye maisha yao ya baadae na taifa kwa ujumla.
Sidhani kama kufanya michezo kama recreation tuu tutajua vipaji vya hawa watoto.
kwani walikuwa na masomo mangapi?
Majaliwa ni nani jamani? Nipo Tz kweli?
masomo 9.
ni wazir katika ofsi ya wazir mkuu anayeshuhulikia Elimu
Ameyasema hayo leo akiwa mkoani Arusha akiongea na wadau wa elimu mkoani humo.Amebainisha kwamba masomo kwa darasa la kwanza yatapunguzwa na kuwa matatu:Kusoma,Kuandika na Kuhesabu (KKK).Source TBC1 Taarifa Saa 2 Usiku
Kwa nini mtoto afikie darasa la pili bila kujua kusoma na kundika?
Vipi akirudia na bado akashindwa kusoma na kuandika? Ataendelea kurudia tuu?
Yaani mwanafunzi asipofaulu arudie darasa ndiyo solution ya kumfanya afaulu?
Na asipofaulu tena, je?
Haya ni mawazo yake au ni kwa mujibu wa Mtaala. Hakuna hata kipindi cha MICHEZO?
Siyo suluhu ya kumfanya afaulu, bali kurudia kutamfanya aelewe. Inawezekana alishindwa kumudu KKK kwa kuwa uwezo wa akili ulikuwa mdogo, hivyo, kama atarudia darasa huku akitiliwa mkazo atamudu KKK.
Ikumbukwe watoto, kama ilivyo kwa watu wazima, wanatofautiana sana katika utendaji kazi wa akili na viungo. Hii ni kwa sababu za kibailojia, kimazingiza, tamaduni n.k.
Hii ilitimiaka mpaka miaka ya tisini mwishoni, nakumbuka ili mwanafunzi aingie darasa la Tatu ilikuwa sharti amudu KKK, pia ili mwanafunzi aingie darasa la Tano sharti aweze orodha ya 1-12. Mitihani ilikuwa inachuja vizuri.
Miaka ya 1990s kulikuwa na idadi ndogo sana, au hakuna kabisa, mwanafunzi anayehutimu Elimu ya Msingi bila ya kumudu kusoma, kuandika, hesabu na maarifa kwa ujumla (kama jografia, sayansi n.k).
ni wazir katika ofsi ya wazir mkuu anayeshuhulikia Elimu
Mbona mawaziri wa elimu wengi bila mpangillio? Kawambwa, Mulugo, Majaliwa. Wanapewa madaraka kama fadhila na kuzidi kuongeza gharama kuwalipa mishahara, posho na magari(shangingi)
Ni kweli mkuu.Ila mgawanyo ni kwamba Kawambwa na Mulugo wanashughulikia Mafunzo (vyuo) na Elimu ya Juu wakati Majaliwa et al. ni Msingi na Sekondari