Siyo suluhu ya kumfanya afaulu, bali kurudia kutamfanya aelewe. Inawezekana alishindwa kumudu KKK kwa kuwa uwezo wa akili ulikuwa mdogo, hivyo, kama atarudia darasa huku akitiliwa mkazo atamudu KKK.
Ikumbukwe watoto, kama ilivyo kwa watu wazima, wanatofautiana sana katika utendaji kazi wa akili na viungo. Hii ni kwa sababu za kibailojia, kimazingiza, tamaduni n.k.
Hii ilitimiaka mpaka miaka ya tisini mwishoni, nakumbuka ili mwanafunzi aingie darasa la Tatu ilikuwa sharti amudu KKK, pia ili mwanafunzi aingie darasa la Tano sharti aweze orodha ya 1-12. Mitihani ilikuwa inachuja vizuri.
Miaka ya 1990s kulikuwa na idadi ndogo sana, au hakuna kabisa, mwanafunzi anayehutimu Elimu ya Msingi bila ya kumudu kusoma, kuandika, hesabu na maarifa kwa ujumla (kama jografia, sayansi n.k).