Waziri Majaliwa: Darasa La Kwanza Kupunguziwa Masomo...

Chipolopolo

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2012
Posts
1,425
Reaction score
726
Ameyasema hayo leo akiwa mkoani Arusha akiongea na wadau wa elimu mkoani humo.Amebainisha kwamba masomo kwa darasa la kwanza yatapunguzwa na kuwa matatu:Kusoma,Kuandika na Kuhesabu (KKK).Source TBC1 Taarifa Saa 2 Usiku
 
Wanatapatapa tu, bila maslahi mazuri kwa walimu hapataeleweka kitu, tushachoka walimu sasa ni passive strike tu.
 
kwani yalikuwa mangapi na yalikuwa yanaitwaje ?, kama yalikuwa hesabu, kingereza, na kiswahili si bado ni kusoma, kuandika na kuhesabu ? haya mambo ni kuleta complications za bure, kazi ya kuelimisha wangeachiwa waalimu na sio wanasiasa
 
Yalikua 12
 
Ameyasema hayo leo akiwa mkoani Arusha akiongea na wadau wa elimu mkoani humo.Amebainisha kwamba masomo kwa darasa la kwanza yatapunguzwa na kuwa matatu:Kusoma,Kuandika na Kuhesabu (KKK).Source TBC1 Taarifa Saa 2 Usiku

Kwa hiyo Tume Ya Mizengo haina kazi. Maana majibu ya tatizo la elimu Tanzania kumbe anayo waziri Majaliwa!! Kweli Nchi hii ni banda la vituko
 
masomo drs la I yapo saba, hesabu, kiingereza. kiswahili, sayansi, stad za kaz, haiba na michezo na tehama
 
sasa wanafunzi wasifundishwe haiba na michezo ?, Tehama je ?, au hawajui kwamba information technology ndio kuandika na kusoma kwa karne hii ?, na kiswahili na kingereza kuna tofauti gani na kusoma ? au hesabu ina tofauti gani na kuhesabu ?, hawa jamaa wanaleta siasa tu, ndio maana nikasema kazi ya kufundisha waachiwe waalimu na wenyewe ndio watoe mapendekezo kipi ni bora na sio wanasiasa
 
kupunguziwa masomo ni halali hata walimu walilipigia sana kelele unakuta mtu hajajua hata kuandika bado tayari kashalundikiwa mzigo mwingine ambao ulitakiwa uwe stage nyingine ambayo ameshajua kusoma na kuandika ilikuwa ni mzigo kwa walimu.
 
Hapo kuna vitu kama Stadi za Kazi au Haiba na Michezo huoni faida yake ?, Hususan michezo inamsaidia ku-refresh ili asiwe bored na shule, after all All work and no play makes Jack a Dull Boy
 
Back
Top Bottom