Waziri Majaliwa: Darasa La Kwanza Kupunguziwa Masomo...

Waziri Majaliwa: Darasa La Kwanza Kupunguziwa Masomo...

hata wakibakiza somo moja haitasaidia kitu bado wengi watamaliza std 7 bila kujua kusoma wala kuandika.

Kwa mtazamo wangu nadhani hii ina nafuu.Darasa la kwanza na la pili mkazo utakuwa Kusoma Kuandika na Kuhesabu (KKK)
 
Wanatapatapa tu, bila maslahi mazuri kwa walimu hapataeleweka kitu, tushachoka walimu sasa ni passive strike tu.

Kweli waboreshe maslahi na ameahidi hilo ikiwa pia kulipa malimbikizo ya waalimu.Ila hatua hii ya mkazo wa KKK inaweza kusaidia,kwa mtazamo wangu
 
kwani yalikuwa mangapi na yalikuwa yanaitwaje ?, kama yalikuwa hesabu, kingereza, na kiswahili si bado ni kusoma, kuandika na kuhesabu ? haya mambo ni kuleta complications za bure, kazi ya kuelimisha wangeachiwa waalimu na sio wanasiasa

Sita mkuu.Hayo pia ni maoni ya wadau wa Elimu
 
Kwa hiyo Tume Ya Mizengo haina kazi. Maana majibu ya tatizo la elimu Tanzania kumbe anayo waziri Majaliwa!! Kweli Nchi hii ni banda la vituko

Tume ile inafanyia kazi sababu za kufeli,mwaka huu na pia itapendekeza hatua za kunusuru ushukaji wa ufaulu.Hii ya KKK ni kwa shule ya Msingi kuwaandaa ili wasiwepo mbumbumbu.
 
Hapo kuna vitu kama Stadi za Kazi au Haiba na Michezo huoni faida yake ?, Hususan michezo inamsaidia ku-refresh ili asiwe bored na shule, after all All work and no play makes Jack a Dull Boy

Usimalo ni kweli lakini ingefaa zaidi wangewanzia wakiwa darasa la tatu wakiwa tayari na msingi wa kujua kusoma na kuandika. Kumbuka mtoto wake mchezo hata akiwa nyumbani. Na wanaposema kuhesabu ni pamoja na kujumlisha na kutoa.
 
Ndinimbya😛amoja sanaa...
 
Last edited by a moderator:
Mwanafunzi asipoweza kusoma na kuandika arudie darasa la Pili. Pia mtihani wa darasa la Nne utiliwe mkazo, yaani mwanafunzi asipofaulu arudie darasa.
 
Mwanafunzi asipoweza kusoma na kuandika arudie darasa la Pili. Pia mtihani wa darasa la Nne utiliwe mkazo, yaani mwanafunzi asipofaulu arudie darasa.

Maoni mazuri hayo mkuu. Bila shaka itapunguza idadi ya wasiojua kusoma na kuandika....
 
Ameyasema hayo leo akiwa mkoani Arusha akiongea na wadau wa elimu mkoani humo.Amebainisha kwamba masomo kwa darasa la kwanza yatapunguzwa na kuwa matatu:Kusoma,Kuandika na Kuhesabu (KKK).Source TBC1 Taarifa Saa 2 Usiku

Hata mchezo hakuna?
 
Mwanafunzi asipoweza kusoma na kuandika arudie darasa la Pili. Pia mtihani wa darasa la Nne utiliwe mkazo, yaani mwanafunzi asipofaulu arudie darasa.

Kwa nini mtoto afikie darasa la pili bila kujua kusoma na kundika?

Vipi akirudia na bado akashindwa kusoma na kuandika? Ataendelea kurudia tuu?

Yaani mwanafunzi asipofaulu arudie darasa ndiyo solution ya kumfanya afaulu?
 
Ukistaajabu ya Mungai
Utaona ya Majariwa

Ccm inaweweseka hawa ndiyo wenye dhamana
ya Elimu yaani masomo yanapunguzwa hawakujua darasa la kwanza na masomo saba
mtoto hatayaweza?
 
Mkuu nina amini kwamba kama waalimu wakitimiza wajibu wao sawasawa miaka miwili yaani darasa la kwanza na la pili kwa kukazia KKK itawezesha wanafunzi kujua kusoma na kuandika
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Ukistaajabu ya Mungai
Utaona ya Majariwa

Ccm inaweweseka hawa ndiyo wenye dhamana
ya Elimu yaani masomo yanapunguzwa hawakujua darasa la kwanza na masomo saba
mtoto hatayaweza?

Mkuu nadhani kwa hili pamoja na madhaifu ya mfumo wetu wa elimu,mpango huu unaweza kusaidia
 
Mwanafunzi asipoweza kusoma na kuandika arudie darasa la Pili. Pia mtihani wa darasa la Nne utiliwe mkazo, yaani mwanafunzi asipofaulu arudie darasa.

Na asipofaulu tena, je?
 
Back
Top Bottom