saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 624
- 1,456
Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema kwenye siasa kuna maneno mengi na unahitaji ngozi ngumu na kifua kwani kila umeme unapokatika jina linaloibwa ni lake.
“Kwenye siasa kuna maneno mengi na unahitaji ngozi ngumu na kifua, kila umeme unapokatika jina lililoimbwa ni la kwangu wala sio TANESCO au wafanyakazi wake, ilifika hatua ikasemwa Rais (Samia Suluhu Hassan) tazama huyu mtu (January)” alisema Januari
“Kuna kocha anaitwa Mourinho napenda staili yake sana, yeye akiwa katika mechi ya ugenini ambayo unakuta uwanja umejaa anakuwa wa kwanza kuingia ndani ya uwanja, anazomewa na mashabiki wa timu pinzani kisha anawaambia wachezaji wake watoke vyumba vya kubadilisha nguo na waingie uwanjani. Ndivyo ilivyokuwa kwangu nilikubali kupokea mashambulizi” alisema Makamba
Chanzo Gazeti la Mwananchi Julai 15, 2022