Waziri Makamba akutana kwa mazungumzo na Waziri wa Viwanda na Teknolojia ya Juu wa Serikali ya UAE

Yale mashirika waliouzia wazawa wakayatelekeza sasa yamefika pake.

Huko Ar ilikuwepo general tairi
huko mbeya ikawepo hi soap, mbeya tex, sido vyombo

Vyote vyote wakapewa watu wakafanya ma godown

Sasa je? Huyu mjomba wa Mheshimiwa kuna kitu atafanya au atanunua viwanda na raia?

And why Arabs only?
And why Arabs only?
[emoji23][emoji23][emoji23]Ni kwa sababu wanapesa lukuki.
 
Hakuna kitu kama hicho !! Bandari ni mali za Nchi wale Dipiwedi ni wawekezaji tu kama wengine waliokuwepo kabla yao !
TICTS and the likes 😅🙏

Maubaguzi hayafai bandugu 🙏🙏🙏
Duuh! Kumbe najadiliana na mtu asiyetumia akili zake! Mkataba wa DPW na TICTS ni sawa?

Siwezi kuwa na ndugu mjinga asiyefundishika nikatulia bila kujali!
 
Hata waheshimiwa wabunge wote waliridhia uwekezaji wa dipiwedi !
Yaani unataka kusema nao hawajui kitu ??!
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amekutana na kuzungumza na Waziri wa Viwanda na Tekinolojia ya Juu wa Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Sultan Ahmed Al Jaber Jijini Nairobi, Kenya.

Waziri Makamba amekutana na Mhe. Al Jaber pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi unaofanyika Nairobi, Kenya.

Pamoja na mambo mengine, Mhe. Waziri Makamba ameihakikishia UAE kuwa Tanzania itashiriki Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 28) mwezi Disemba 2023, ambapo miongoni mwa masuala itakayoyatilia mkazo ni ufadhili wa miradi ya nishati safi ya kupikia kwa akina mama vijijini.

Aidha, Mheshimiwa Waziri Makamba amesisitiza kuwa Tanzania itaungana na nchi za Afrika na nchi nyingine zinazoendelea duniani, kuhimiza Nchi Wanachama, hususan zilizoendelea kutekeleza ahadi za kupunguza hewa ukaa, kuchangia fedha kwa ajili ya Uhimilivu na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi na upatikanaji wa teknolojia kwa ajili ya jitihada hizo.

Kwa upande wake, Mhe. Sultan Ahmed Al Jaber, aliishukuru Tanzania kwa kuahidi kushiriki Mkutano wa COP 28 na kwamba Umoja wa Falme za Kiarabu umejipanga kuhakikisha Mkutano wa COP 28 unaleta matokeo chanya katika jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi Duniani.

Aidha, Mhe. Al Jaber aliahidi kuunga mkono masuala ya kipaumbele ya Tanzania katika Mkutano huo kwa kuzingatia uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na UAE.

Mhe. Al Jaber ni Rais ajaye wa Mkutano wa Cop 28 unaotarajiwa kufanyika Dubai, mwezi Disemba 2023.

#newsupdatemedia2023View attachment 2743874
Pia soma

Mabadiliko Mawaziri tuliingizwa Kingi
Amepelekwa kulinda maslahi ya maza kwa waarabu
 
Waarabu sio watu wazuri, wametutesa Sana biashara ya utumwa, tukae nao mbali #okoa bandari #Okoa Ngorongoro #okoa Misitu
 
Sijakuelewa hapo kuna tatizo gani?

Au ulifikiri Makamba alikwenda kucheza Nairobi?
 
Back
Top Bottom