Waziri Makamba: Umeme utaendelea kukatika mpaka tumalize maboresho. TPSF wamshukia kama mwewe

Kiturilo

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
708
Reaction score
2,859
Waziri wa Nishati, January Makamba amesema changamoto ya kukatika kwa umeme itaendelea kuwepo, hadi pale marekebisho na maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika yatakapokamilika.

Miongoni mwa maboresho hayo ni kujenga na kurekebisha njia za umeme na kuimarisha vituo vya kupooza umeme na transfoma, hatua aliyosema italeta ufanisi na uimara katika usambazaji wa nishati hiyo katika maeneo mbalimbali nchini.

Hata hivyo, taarifa hiyo haijawavutia wadau wa sekta hiyo kama vile Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI), waliosema kuwa ni taarifa mbaya na kwamba uzalishaji unaweza kupungua.

Makamba alieleza hayo juzi alipokuwa akizungumzia mafanikio ya mwaka mmoja wa wizara hiyo, katika mkutano uliofanyika katika studio za kituo cha runinga cha Azam. Mkutano huo uliohudhuriwa na wahariri wa vyombo vya habari pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu.

“Maswali ni mengi umeme, umeme…nataka nisema kwamba hadi pale tutakapomaliza kazi yetu ya kukarabati, kubadilisha, kurekebisha. Bado tutaendelea kukabiliana na changamoto ya kukatika kwa umeme kwa sababu ni sayansi sio maneno.

“Kwenye umeme kuna njia za kuusafirisha ambazo ni kv 400,220, 132 na 66; za kusambaza umeme ni 33 na 11.Kuna kikomo cha 11 kinachotakiwa kupeleka umeme kilomita 30 na 33 au 100. Njia ya kutoka Mkuranga hadi Lindi ni umeme wa mtaani,ambapo njia ya kilomita 400 sasa unategemea nini mtu akijenga kiwanda hapo,” alisema.

Makamba alisema hivi sasa Serikali inabadilisha njia zote za umeme zilizozidiwa, akisema mchakato utachukua muda kidogo na kwamba hataki kuonekana muongo kwa Watanzania.

“Lazima tuwekeze na Serikali ya awamu ya sita inalifanya hilo, nia yetu kazi hii ifanyike ndani ya miaka miwili kwa kadri rasilimali zitakavyopatikana kwa sababu mahitaji ya umeme hivi sasa yamekuwa makubwa tofauti na miaka iliyopita,”alisema.

Katika mkutano huo, Makamba alitumia grafu kuonesha namna mahitaji ya nishati hiyo yalivyopungua na kuongezeka kwa nyakati tofauti kuanzia mwaka 2011 hadi 2013, akisema kulikuwa na ongezeko la watumiaji wengi wa nishati hiyo.

Hata hiyo, Makamba alisema mwaka 2014 kulikuwa na kupanda na kushuka lakini kati ya 2016/17 mahitaji ya umeme yalishuka kwa asilimia tisa, akisema lilikuwa jambo la kushangaza kwa Taifa lenye shughuli mbalimbali. Alisema mahitaji yalipungua kwa sababu shughuli za uzalishaji zilishuka.
“Kwa sasa nchi imefunguka na uzalishaji umeongezeka,” alisema Makamba ambaye pia mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga.

“Serikali inafanya kazi tatu kwa mpigo ikiwemo kurebisha mifumo, kwenye transfoma na njia za umeme zilizochoka na kuchakaa. Tunaongeza uzalishaji ikiwemo kuweka miundombinu mipya ya kupeleka umeme maeneo mengi zaidi na kulisuka upya Tanesco (Shirika la Umeme Tanzania), ili litekeleze majukumu yake kwa ufanisi,” alisema

Makamba alisema ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia, wizara hiyo imetekeleza masuala mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya kimfumo, rasilimali watu, kutafuta fedha, kutengeneza mifumo mipya ya mipango mikakati ili taasisi za wizara hiyo zifanye kazi kwa ufanisi.

“Kwa kipindi tutakachoshika dhamana hii, tutatumia mbinu, maarifa na uwezo wote ili kutekeleza yote yanayopaswa kufanyika. Hatutawadanganya Watanzania kuhusu yaliyopo, tukifanya hivyo, tutakuja kuumbuka huko mbele na hatutazitendea haki nafasi tulizopewa,” alisema Makamba.

Alisema malengo ya Serikali ni kufikisha megawati 5,000 ifikapo mwaka 2025, lakini ndani ya mwaka mmoja wizara hiyo, imeanzisha na kubuni miradi ukiwemo wa Sh 4trilioni utakaodhibiti changamoto za kukatika kwa umeme. Kwa mujibu wa Makamba tayari wamepewa Sh400 bilioni ili kuimarisha gridi ya Taifa.

Pia, alieleza sababu za Serikali za kutouza umeme nje ya nchi akisema: “Kuuza umeme nje, lazima uwe na umeme unaojitolesheza kwa watu wako; sasa tuna megawati 1,700.Tutosheleze kwanza mahitaji yetu, kisha umeme wa ziada tuingize kwenye masoko ya pamoja.

Kilio cha wadau

Akizungumzia tatizo la kukatika umeme katika uzalishaji, Mkurugenzi wa Sera, Utafiti na Utetezi wa Taasisi ya Sekta binafsi (TPSF), Andrew Mahiga alisema hiyo ni habari mbaya kwao kwani uzalishaji utashuka.

“Ni wazi kwamba uzalishaji utashuka, kwa sababu kama mtu alikuwa anazalisha kwa saa 12, itabidi azalishe kwa saa sita kwa kukosa umeme wa kuendesha mitambo au kuhifadhi bidhaa au wakati mwingine mtu analazimika kununua mafuta ili kuendeshea mitambo, hivyo gharama itaongezeka,” alisema Mahiga.

Alisema wamekuwa wakizungumza na Serikali kuhusu changamoto za uzalishaji ikiwemo ya umeme.

“Kuna shida ya umeme, miundombinu, tozo, hizo zote ni changamoto za uzalishaji. Masuala ya umeme siyo gharama kubwa, ni ile consistence (mwendelezo), Kama umeme ungekuwa unawaka saa 24 hakutakuwa na malalamiko. Au kama umeme unakuja kwa nguvu inayotakiwa, kuna siku umeme unakuja mdogo na siku nyingine mkubwa sana, unaweza kuharibu mashine,’’ alisema.

Naye Ofisa sera na biashara wa Shirikisho la Viwanda (CTI), Frank Dafa aliungana na TPSF akisema kutakuwa na athari kubwa.

“Kuathirika ni lazima, kwa sababu kuna watu tuliwatembelea tukawauliza wakasema bado umeme unakatika. Kwa hiyo suluhisho ni kutumia nishati mbadala kama mafuta, lakini kwa kuwa nayo yamepanda bei gharama inaongezeka.

“Halafu kuna vifaa nyeti kwenye mitambo, endapo umeme utakuja mdogo vinaungua wakati mwingine, kwa hiyo inabidi wanunue vingine na ni gharama kubwa na ukiangalia gharama za kusafirisha mizigo, inaweza kusababisha kusimamisha uzalishaji,” alisema Dafa.

Hata hivyo, alisema wamekuwa wakiihusisha Tanesco na imekuwa ikiwapa ushirikiano.

“Wamegawa maeneo katika kanda na wameanzisha makundi ya WhatsApp kwa hiyo kukiwa na changamoto unaiweka huko, kama wanaiweza wanaitatua, kama iko nje ya uwezo wao, ndio basi tena,” alisema.

Alisema licha ya tatizo hilo kutosababisha kufungwa kwa viwanda, changamoto ya umeme inapunguza imani ya wawekezaji

“Uhakika wa umeme ni kigezo kikubwa cha uwekezaji, japo sio pekee. Kuna watu wanatumia mashine nyingi, angetaka kuwa na umeme wa kutosha. Kama watu walio kwenye uzalishaji wa vyakula watakuwa na friji nyingi,” alisema.

Alitaja pia kuwapo kwa changamoto ya kutofidiwa kwa uharibifu wa vifaa, unaotokana na kukatika kwa umeme.

“Kuna pendekezo la zamani siku hizi silioni; ambalo ni kuwa na mkataba kati ya mtoa huduma na mtumiaji, ili kwamba ikitokea umeme umekatika kwa sababu ya uzembe wa mtoa huduma, amfidie. Kwa hiyo kikubwa tunachopendekeza ni mifumo iboreshwe kwa sababu mingi imechakaa,” alisema.

Bei ya gesi kupanda

Kuhusu upandaji wa bei ya gesi mara kwa mara, Makamba alisema hatua hiyo inatokana na sababu mbalimbali ikiwemo miundombinu ya uingizaji na upakuaji nishati hiyo, bandarini kutokuwa na rafiki.

“Unapoingiza kwa ‘bulk’ kwa kiwango kikubwa bei inakua chini, ukiingiza kidogo kidogo bei inakuwa juu.Miundombinu yetu pole bandari meli ya gesi inayoweza kushusha mzigo ni tani saba, lakini kuna nchi nyingine meli ya hadi ya tani 100,000 inaingia na kushusha mafuta yanayohifadhiwa.

“Kuna changamoto ya miundombinu ya ushushaji na upakuaji, meli zinazoleta gesi ni ndogo ndogo kwa hiyo hata bei zake zinakuwa mtihani kidogo. Suala jingine ni muundo wa biashara wa usambazaji wa gesi yenyewe,” alisema Makamba.

Hata hivyo, Makamba alisema Serikali inafanya upanuzi wa miundombinu bandari, akisema tayari mwekezaji ameshapatikana kwa ajili ya mchakato huo, utakaowezesha meli za tani za 40 kushusha gesi itakayoleta ahueni kwa wananchi.

Gesi ya LNG

Kuhusu wa mradi wa gesi ya kimiminika (Liquefied Natural Gas-LNG),Makamba alisema utakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa kwa sababu utaingiza uwekezaji wa takribani Sh 70 trilioni, akisema mchakato huo unamfurahisha na kumtisha.

“Unanifurahisha kwa sababu utakwenda kubadilisha taswira ya nchi. Mradi huu utajengwa kwa miaka minne hadi sita na wafanyakazi wake hawatapungua 16,000,” alisema Makamba.

“Thamani ya manunuzi kuanzia ujenzi, mafuta, huduma za fedha na vyakula vitapanda katika eneo husika.Kuna kazi zitakazotekelezwa na wazawa, lakini wengine watapata ujuzi utakaowasaidia kufanya kazi katika nchi nyingine baada ya mradi kukamilika,” alisema Makamba.

Makamba alisema hadi sasa majadiliano kuhusu LGN yanakwenda vizuri na wamefika mahali ambapo hawakuwahi kufika, akibainisha kuwa hayo ni mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita.

“Katika mazungumzo yetu tumefikia hatua ya ‘project commercial structure’ kitu ambacho hatukuwahi kukubaliana tangu kuanza mchakato huu. Project commecial structure ndio inaamua masuala ya fedha, kodi na kiufundi,” alisema Makamba.

Mbali na hilo, Makamba alisema Serikali inajenga chuo kipya cha masuala ya mafuta na gesi mkoani Mtwara, ili kukuza ujuzi wa sekta hiyo, akisema vigezo na taratibu za vijana wanaotakiwa kusoma zitatangazwa kwenye bajeti ya wizara hiyo ya mwaka wa fedha 2022/2023.
 
Waziri wangu Makamba hongera na pole kwa majukumu mazito ya wizara hii, fikiria kuyafanya haya ili kupunguza athari za umeme kukatika;watumiaji wote wa umeme yaani kuanzia Taasisi ya Urais hadi kwetu huku Lingusenguse walipe kupata umeme,hakuna umeme wa bure;umeme wote unaopotea kwenye mzunguko uthibitiwe, tunaweza kutumia well trained technicians na miundo mbinu ya kisasa na imara,;tuzalishe umeme rafiki hasa wa upepo, solar na nyukilia (ingawa huu inahitajika uwekezaji mkubwa);

Fanya ziara pale 🇹🇷 na ukifunze wenzetu wanavyotumia meli maalum kuzalisha umeme, tukifanikiwa kupata meli 5 na back up kama 3 hivi, zika dock kwenye bandari zetu,mfano mtwara 1,visiwani 1,Dar 2 na tanga 1,hizi meli zinaweza kuzalisha zaidi ya 1400MW za umeme,ambao utasaidia mno kuondoa tatizo la umeme, always be smart usitumie nguvu au politics, issue ya umeme ni uti wa mgongo wa uchumi wetu,good luck
 
Waziri wangu Makamba hongera na pole kwa majukumu mazito ya wizara hii, fikiria kuyafanya haya ili kupunguza athari za umeme kukatika;watumiaji wote wa umeme yaani kuanzia Taasisi ya Urais hadi kwetu huku Lingusenguse walipe kupata umeme,hakuna umeme wa bure;umeme wote unaopotea kwenye mzunguko uthibitiwe, tunaweza kutumia well trained technicians na miundo mbinu ya kisasa na imara,;tuzalishe umeme rafiki hasa wa upepo, solar na nyukilia (ingawa huu inahitajika uwekezaji mkubwa);Fanya ziara pale 🇹🇷 na ukifunze wenzetu wanavyotumia meli maalum kuzalisha umeme, tukifanikiwa kupata meli 5 na back up kama 3 hivi, zika dock kwenye bandari zetu,mfano mtwara 1,visiwani 1,Dar 2 na tanga 1,hizi meli zinaweza kuzalisha zaidi ya 1400MW za umeme,ambao utasaidia mno kuondoa tatizo la umeme, always be smart usitumie nguvu au politics, issue ya umeme ni uti wa mgongo wa uchumi wetu,good luck

Umetaja meli, lakiji unajua huko kwenye meli huo umeme unazalishwa na nini? source of power namaanisha...
 
Muda siyo mrefu utasema hakuna elimu ya bure.

Mkishiba mnakuwa wajinga sana
Ukiongea politics tutaharibu mada,hakuna free lunch hapa duniani, elimu ya bure ipo wapi?mimi siioni kuwa kuna elimu bure hapa nchini, awamu ya kwanza kutokana na political will, mipango mizuri ya serikali ile, idadi ndogo (manageable)ya wanafunzi yeah elimu ilikua kama unavyosema
 
Waziri wa Nishati, January Makamba amesema changamoto ya kukatika kwa umeme itaendelea kuwepo, hadi pale marekebisho na maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika yatakapokamilika.

Miongoni mwa maboresho hayo ni kujenga na kurekebisha njia za umeme na kuimarisha vituo vya kupooza umeme na transfoma, hatua aliyosema italeta ufanisi na uimara katika usambazaji wa nishati hiyo katika maeneo mbalimbali nchini.

Hata hivyo, taarifa hiyo haijawavutia wadau wa sekta hiyo kama vile Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI), waliosema kuwa ni taarifa mbaya na kwamba uzalishaji unaweza kupungua.

Makamba alieleza hayo juzi alipokuwa akizungumzia mafanikio ya mwaka mmoja wa wizara hiyo, katika mkutano uliofanyika katika studio za kituo cha runinga cha Azam. Mkutano huo uliohudhuriwa na wahariri wa vyombo vya habari pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu.

“Maswali ni mengi umeme, umeme…nataka nisema kwamba hadi pale tutakapomaliza kazi yetu ya kukarabati, kubadilisha, kurekebisha. Bado tutaendelea kukabiliana na changamoto ya kukatika kwa umeme kwa sababu ni sayansi sio maneno.

“Kwenye umeme kuna njia za kuusafirisha ambazo ni kv 400,220, 132 na 66; za kusambaza umeme ni 33 na 11.Kuna kikomo cha 11 kinachotakiwa kupeleka umeme kilomita 30 na 33 au 100. Njia ya kutoka Mkuranga hadi Lindi ni umeme wa mtaani,ambapo njia ya kilomita 400 sasa unategemea nini mtu akijenga kiwanda hapo,” alisema.

Makamba alisema hivi sasa Serikali inabadilisha njia zote za umeme zilizozidiwa, akisema mchakato utachukua muda kidogo na kwamba hataki kuonekana muongo kwa Watanzania.

“Lazima tuwekeze na Serikali ya awamu ya sita inalifanya hilo, nia yetu kazi hii ifanyike ndani ya miaka miwili kwa kadri rasilimali zitakavyopatikana kwa sababu mahitaji ya umeme hivi sasa yamekuwa makubwa tofauti na miaka iliyopita,”alisema.

Katika mkutano huo, Makamba alitumia grafu kuonesha namna mahitaji ya nishati hiyo yalivyopungua na kuongezeka kwa nyakati tofauti kuanzia mwaka 2011 hadi 2013, akisema kulikuwa na ongezeko la watumiaji wengi wa nishati hiyo.

Hata hiyo, Makamba alisema mwaka 2014 kulikuwa na kupanda na kushuka lakini kati ya 2016/17 mahitaji ya umeme yalishuka kwa asilimia tisa, akisema lilikuwa jambo la kushangaza kwa Taifa lenye shughuli mbalimbali. Alisema mahitaji yalipungua kwa sababu shughuli za uzalishaji zilishuka.

Advertisement

“Kwa sasa nchi imefunguka na uzalishaji umeongezeka,” alisema Makamba ambaye pia mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga.

“Serikali inafanya kazi tatu kwa mpigo ikiwemo kurebisha mifumo, kwenye transfoma na njia za umeme zilizochoka na kuchakaa. Tunaongeza uzalishaji ikiwemo kuweka miundombinu mipya ya kupeleka umeme maeneo mengi zaidi na kulisuka upya Tanesco (Shirika la Umeme Tanzania), ili litekeleze majukumu yake kwa ufanisi,” alisema

Makamba alisema ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia, wizara hiyo imetekeleza masuala mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya kimfumo, rasilimali watu, kutafuta fedha, kutengeneza mifumo mipya ya mipango mikakati ili taasisi za wizara hiyo zifanye kazi kwa ufanisi.

“Kwa kipindi tutakachoshika dhamana hii, tutatumia mbinu, maarifa na uwezo wote ili kutekeleza yote yanayopaswa kufanyika. Hatutawadanganya Watanzania kuhusu yaliyopo, tukifanya hivyo, tutakuja kuumbuka huko mbele na hatutazitendea haki nafasi tulizopewa,” alisema Makamba.

Alisema malengo ya Serikali ni kufikisha megawati 5,000 ifikapo mwaka 2025, lakini ndani ya mwaka mmoja wizara hiyo, imeanzisha na kubuni miradi ukiwemo wa Sh 4trilioni utakaodhibiti changamoto za kukatika kwa umeme. Kwa mujibu wa Makamba tayari wamepewa Sh400 bilioni ili kuimarisha gridi ya Taifa.

Pia, alieleza sababu za Serikali za kutouza umeme nje ya nchi akisema: “Kuuza umeme nje, lazima uwe na umeme unaojitolesheza kwa watu wako; sasa tuna megawati 1,700.Tutosheleze kwanza mahitaji yetu, kisha umeme wa ziada tuingize kwenye masoko ya pamoja.

Kilio cha wadau

Akizungumzia tatizo la kukatika umeme katika uzalishaji, Mkurugenzi wa Sera, Utafiti na Utetezi wa Taasisi ya Sekta binafsi (TPSF), Andrew Mahiga alisema hiyo ni habari mbaya kwao kwani uzalishaji utashuka.

“Ni wazi kwamba uzalishaji utashuka, kwa sababu kama mtu alikuwa anazalisha kwa saa 12, itabidi azalishe kwa saa sita kwa kukosa umeme wa kuendesha mitambo au kuhifadhi bidhaa au wakati mwingine mtu analazimika kununua mafuta ili kuendeshea mitambo, hivyo gharama itaongezeka,” alisema Mahiga.

Alisema wamekuwa wakizungumza na Serikali kuhusu changamoto za uzalishaji ikiwemo ya umeme.

“Kuna shida ya umeme, miundombinu, tozo, hizo zote ni changamoto za uzalishaji. Masuala ya umeme siyo gharama kubwa, ni ile consistence (mwendelezo), Kama umeme ungekuwa unawaka saa 24 hakutakuwa na malalamiko. Au kama umeme unakuja kwa nguvu inayotakiwa, kuna siku umeme unakuja mdogo na siku nyingine mkubwa sana, unaweza kuharibu mashine,’’ alisema.

Naye Ofisa sera na biashara wa Shirikisho la Viwanda (CTI), Frank Dafa aliungana na TPSF akisema kutakuwa na athari kubwa.

“Kuathirika ni lazima, kwa sababu kuna watu tuliwatembelea tukawauliza wakasema bado umeme unakatika. Kwa hiyo suluhisho ni kutumia nishati mbadala kama mafuta, lakini kwa kuwa nayo yamepanda bei gharama inaongezeka.

“Halafu kuna vifaa nyeti kwenye mitambo, endapo umeme utakuja mdogo vinaungua wakati mwingine, kwa hiyo inabidi wanunue vingine na ni gharama kubwa na ukiangalia gharama za kusafirisha mizigo, inaweza kusababisha kusimamisha uzalishaji,” alisema Dafa.

Hata hivyo, alisema wamekuwa wakilihusisha Tanesco na limekuwa likiwapa ushirika.

“Wamegawa maeneo katika kanda na wameanzisha makundi ya WhatsApp kwa hiyo kukiwa na changamoto unaiweka huko, kama wanaiweza wanaitatua, kama iko nje ya uwezo wao, ndio basi tena,” alisema.

Alisema licha ya tatizo hilo kutosababisha kufungwa kwa viwanda, changamoto ya umeme inapunguza imani ya wawekezaji

“Uhakika wa umeme ni kigezo kikubwa cha uwekezaji, japo sio pekee. Kuna watu wanatumia mashine nyingi, angetaka kuwa na umeme wa kutosha. Kama watu walio kwenye uzalishaji wa vyakula watakuwa na friji nyingi,” alisema.

Alitaja pia kuwapo kwa changamoto ya kutofidiwa kwa uharibifu wa vifaa, unaotokana na kukatika kwa umeme.

“Kuna pendekezo la zamani siku hizi silioni; ambalo ni kuwa na mkataba kati ya mtoa huduma na mtumiaji, ili kwamba ikitokea umeme umekatika kwa sababu ya uzembe wa mtoa huduma, amfidie. Kwa hiyo kikubwa tunachopendekeza ni mifumo iboreshwe kwa sababu mingi imechakaa,” alisema.

Bei ya gesi kupanda

Kuhusu upandaji wa bei ya gesi mara kwa mara, Makamba alisema hatua hiyo inatokana na sababu mbalimbali ikiwemo miundombinu ya uingizaji na upakuaji nishati hiyo, bandarini kutokuwa na rafiki.

“Unapoingiza kwa ‘bulk’ kwa kiwango kikubwa bei inakua chini, ukiingiza kidogo kidogo bei inakuwa juu.Miundombinu yetu pole bandari meli ya gesi inayoweza kushusha mzigo ni tani saba, lakini kuna nchi nyingine meli ya hadi ya tani 100,000 inaingia na kushusha mafuta yanayohifadhiwa.

“Kuna changamoto ya miundombinu ya ushushaji na upakuaji, meli zinazoleta gesi ni ndogo ndogo kwa hiyo hata bei zake zinakuwa mtihani kidogo. Suala jingine ni muundo wa biashara wa usambazaji wa gesi yenyewe,” alisema Makamba.

Hata hivyo, Makamba alisema Serikali inafanya upanuzi wa miundombinu bandari, akisema tayari mwekezaji ameshapatikana kwa ajili ya mchakato huo, utakaowezesha meli za tani za 40 kushusha gesi itakayoleta ahueni kwa wananchi.

Gesi ya LNG

Kuhusu wa mradi wa gesi ya kimiminika (Liquefied Natural Gas-LNG),Makamba alisema utakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa kwa sababu utaingiza uwekezaji wa takribani Sh 70 trilioni, akisema mchakato huo unamfurahisha na kumtisha.

“Unanifurahisha kwa sababu utakwenda kubadilisha taswira ya nchi. Mradi huu utajengwa kwa miaka minne hadi sita na wafanyakazi wake hawatapungua 16,000,” alisema Makamba.

“Thamani ya manunuzi kuanzia ujenzi, mafuta, huduma za fedha na vyakula vitapanda katika eneo husika.Kuna kazi zitakazotekelezwa na wazawa, lakini wengine watapata ujuzi utakaowasaidia kufanya kazi katika nchi nyingine baada ya mradi kukamilika,” alisema Makamba.

Makamba alisema hadi sasa majadiliano kuhusu LGN yanakwenda vizuri na wamefika mahali ambapo hawakuwahi kufika, akibainisha kuwa hayo ni mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita.

“Katika mazungumzo yetu tumefikia hatua ya ‘project commercial structure’ kitu ambacho hatukuwahi kukubaliana tangu kuanza mchakato huu. Project commecial structure ndio inaamua masuala ya fedha, kodi na kiufundi,” alisema Makamba.

Mbali na hilo, Makamba alisema Serikali inajenga chuo kipya cha masuala ya mafuta na gesi mkoani Mtwara, ili kukuza ujuzi wa sekta hiyo, akisema vigezo na taratibu za vijana wanaotakiwa kusoma zitatangazwa kwenye bajeti ya wizara hiyo ya mwaka wa fedha 2022/2023.
Ndio ukweli huo,hao tpsf watoe pesa basi kama wanataka umeme usikatike.

Ikumbukwe mifumo ya umeme imezidiwa na Kuna Kati ya transfer 27,000 zilizopo zaidi ya transfer 10,000 zinatakiwa kubadilisha zote.

Pili matengenezo kiujumla yanahitaji zaidi ya til.4 Ili umeme urejee vizuri.

Screenshot_20220327-111738.png
 
ni bora aseme ukweli kuliko kuwapiga uongo halafu baada tumbebeshe tunguli...
Na ndicho kaongea hata kama inauma,Miaka 6 iliyopita licha ya uchumi kushuka lakini Tanesco haiku repair mitambo ikawa busy na Bwawa la Nyerere matokeo yake uchumi ulivyofunguka demand ya umeme imeongezeka na mitambo imezidiwa.
 
Leta suluhisho au jitokeze tukuteue wewe ukazuie kukatika kwa umeme.
Kama umeme ulikuwa haukatiki kipindi cha Magufuli maana yake suruhisho lipo.

Hawa wanafanya ujanja ujanja tu. Wanakamatwa na wahindi ili wahindi wauze majenereta.

Hata Magufuli alisema. Mimi siwezi kupata huo uteuzi. Ila tumrudishe Keleman haraka kwenye hiyo nafasi
 
Back
Top Bottom