Waziri Makamba: Umeme utaendelea kukatika mpaka tumalize maboresho. TPSF wamshukia kama mwewe

Waziri Makamba: Umeme utaendelea kukatika mpaka tumalize maboresho. TPSF wamshukia kama mwewe

Matengenezo ya kila siku toka uingie kwenye hiyo nafasi?. Ndio matengenezo gani hayo?. Hata kipindi cha Magu matengenezo yalikuwepo. Lakini sio kama hayo yenu
Amesema kwa miaka sita hayakufanyika.

Simtetei but if ni kweli basi mitambo iliyopo lazima iwe overloaded
 
Ndio ukweli huo,hao tpsf watoe pesa basi kama wanataka umeme usikatike.

Ikumbukwe mifumo ya umeme imezidiwa na Kuna Kati ya transfer 27,000 zilizopo zaidi ya transfer 10,000 zinatakiwa kubadilisha zote.

Pili matengenezo kiujumla yanahitaji zaidi ya til.4 Ili umeme urejee vizuri.

KView attachment 2165895
Kwani siku zote huu ukarabati ulikuwa wamsubiri Makamba?

Au ndio ile tabia ya kujiona yeye yuko bright sana na kukunja nne.
 
Kwani siku zote huu ukarabati ulikuwa wamsubiri Makamba? Au ndio ile tabia ya kujiona yeye yuko bright sana na kukunja nne.
Umeelewa kwamba haukufanyika miaka 6 yote? Umeelewa kwamba demand imeongezeka zaidi kwa kukua kwa Uchumi kuliko awamu iliyopita?

Una uhakika wewe ukiteuliwa utadhibiti umeme kukatika?
 
Umeelewa kwamba haukufanyika miaka 6 yote? Umeelewa kwamba demand imeongezeka zaidi kwa kukua kwa Uchumi kuliko awamu iliyopita?

Una uhakika wewe ukiteuliwa utadhibiti umeme kukatika?
Bro hao wanaofanya ukarabati na Makamba sasa, walikuwa mtaani na wakaingizwa kazini alipoteuliwa Makamba? Tuache uongo.
 
Kwani wewe ndio kipimo cha kuwakubali mawaziri? [emoji2][emoji2]

Mlaumuni Mwendazake aliyewekeza kwenye Bwawa bila repair na aliyeharibu uchumi haya ndio madhara yake.

Hali hii ndio ilimkumba JK kwa sababu MKapa hakufanywa uwekezaji kwenye umeme mahitaji makubwa yakatokea awamu ya 4 matokeo yake ni umeme wa dharura wa majenereta.
Mzee lazima unamaslahi na huyu mtu. Mbona kila msg una jibu. Kuna hela unapokea ?
 
Wachukue $1.9 ambazo ni karibia trillion 5 si tri 4, ila hii mbinu ya kuchezea stability ya umeme kujustify hiyo gharama ya maboresho na uchakafu inayo waumiza wananchi waache kuitumia.

Hamna theory yeyote ya kisanyansi itakakayotumiwa ihalalishe kuwa umeme ulisubiri JPM afe na Mh Waziri Makamba awe madarakani ndio miundo mbinu ya TANESCO ihitaji 5Trillion.

Waelezee kisanyansi kwa nini muda mfupi tu baada ya JPM kuchukua nchi tatizo la umeme lilipotea. Mitambo/miundombinu ya Tanesco ilimuogopa JPM?
 
Umeme utaendelea kukatika mpaka amalize muda wake hilo halina ubishi.
 
  • Thanks
Reactions: ALT
Kuna muda unajizuia usiongee lakini inakwaza.

Wananchi wako kimya, hawaoneshi kwa vitendo kusikitishwa na hali ya kukatika kwa umeme, maisha kupanda gharama katika nyanja zote.

Karibia kila kitu kinategemea umeme. Bila ya umeme hakuna ajira viwandani. Kuna kiwanda flani nakihifadhi jina, kimeshusha uzalishaji na kuondoa watu 120 kazini. Jambo baya sana.

Hawa watu 120 walikua na watu wengi sana nyuma yao wanawategemea. Watu hawa wanaishije? Watu hawa waliambiwa umeme ukikaa sawa wataitwa kazini, sasa ni kauli ya baada ya miaka 2.

Hivi watanzania, tuna akili timamu kweli? Mtu mmoja anajiita waziri, umeme ukatike usikatike auathiri mshahara wake, tunakubali kauli za kizembe namna hiyo.

Ifike hatua, nayeye awajibike. Umeme ukikatika, asilipwe mshahara. Kashindwa kusimamia wizara.

Bila nishati ya umeme hakuna maendeleo, taifa lolote lile.

Kwa kauli aliyotoa leo, ningekua mwenye nchi, ningetengua uteuzi wake.

Hopeless and rubbish.
Atafutwe mtaalamu wa umeme ndani ya shirika la tanesco, apewe wizara, tuone kama kutakua na shida. Mhandisi ana njia mbadala za kufanya kazi na matengenezo huku huduma ya umeme ikiwa palepale.

Watu wafanye marekebisho usiku, mchana uzalishaji viwandani uendelee. Watu wapate ajira, uchumi ukue.
 
Okay hata hayo maboresho yakitumia miaka kumi ijayo...

Kama anavyosema umeme ni sayansi sio maneno....

Hivyo basi bora waje wenye maneno wasiotumia sayansi iwapo umeme utakuwa wa uhakika..., Hiyo Sayansi yake ya kukata umeme abaki nayo....

Na mimi nasema UMEME ni Nishati inayotakiwa Kuwaka na Sio Kukatika wala Maneno
 
Tatizo serikali inalazimisha kufanya hii biashara peke yake (monopoly), serikali imejaa mafisadi tuu, hawana pesa wala utaalam wa kuhudumia watu zaidi ya milion 60, waruhusu tuu private sector wazalishe na wasambaze moja kwa moja kwa wananchi,

kazi yao iwe policy tuu na kuhakikisha fair game kati ya wawekezaji na wananchi, tunajidanganya kufikiri Makamba atatuletea umeme Tanzania, tuachane na sheria zinazotufanya maskini na watumwa
 
umetaja meli, lakiji unajua huko kwenye meli huo umeme unazalishwa na nini? source of power namaanisha...
Yes source of power 🔋 inaweza kuwa ni gas (anbayo tunayo ya kutosha, zile za diesel zipo out of our touch, mafuta kwa bei ya sasa itatusumbua mno)
 
Bei ya private sector utaiweza?
Nani kakuambia serikali ndio itakupa umeme wa bei rahisi na sijui kwanini unaamini hivyo maana hatujawahi kuuona kwa zaidi ya miaka 50 TANESCO ilipoanza , nchi nyingi tuu sector ya umeme ni private sector na bei ipo chini na umeme wa kuaminika kuliko hao TANESCO, mlisema same thing kuhusu makampuni ya simu, acheni mawazo ya kitumwa
 
Back
Top Bottom