Waziri Makamba: Umeme utaendelea kukatika mpaka tumalize maboresho. TPSF wamshukia kama mwewe

Tumia akili sio hisia ,umeambiwa miaka 6 hakuna repair ilifanyika,umeambiwa uchumi wa ulikuwa umeanguka miaka ya Mwendazake hivyo mahitaji ya umeme yalikuwa chini na mwisho umeambiwa uchumi umeongezeka zaidi kwa hivyo loading imeongezeka na suluhisho ni kufanya repair na estimates zimewekwa.
 
Kabisa ni kinyaa. Huyu na wa fedha sijawahi kuwakubali. Wameweka maslahi yao mbele
Kwani wewe ndio kipimo cha kuwakubali mawaziri? 😃😃

Mlaumuni Mwendazake aliyewekeza kwenye Bwawa bila repair na aliyeharibu uchumi haya ndio madhara yake.

Hali hii ndio ilimkumba JK kwa sababu MKapa hakufanywa uwekezaji kwenye umeme mahitaji makubwa yakatokea awamu ya 4 matokeo yake ni umeme wa dharura wa majenereta.
 
Mbona maelezo ya Waziri yako clear?

Hawa TPSF wenye uelewa mdogo hivi watatufikisha kokote kweli?
 
Unampigia pande mwizi makatani. Ninavyo vipimo vya kuwapima. Ndio maana hata Magu alimpiga pembeni huyu (sijui ndio wewe mwenyewe utajijua).

Siwezi kumlaumu Magu kwa hicho unachotaka nimlaumu. Yeye alitekeleza wajibu wake ipasavyo. Na alituhakikishia umeme hautakatikati,na alisema kabisa tutaanza kuuza umeme nje. Na alikuwa anamaanisha sio hizo blah blah zako.

Mara ujishow na helicopter. Pamoja na mbwembwe na helicopters hakuna ulichotubadirishia.

Mimi kipindi cha Magu niliuza hata na jenerata langu ksbb umeme ulikuwa wa uhakika. Nilimuingizia umeme mpaka bibiangu kijijini ksbb umeme ulikuwa 27000 tu kuingiza.
 
Magu ndio kipimo? Alimpiga pembeni kwa sababu alitaka aweke ndugu yake wa kusema uongo na kuiba nothing else.

Kwani Vijijini kuingiza umeme Kwa 27,000 kumeisha? Wewe ndio una bibi peke yako? 😁😁.

Ukweli mchungu ni kwamba mwendazake hakufanya repair ndiovyo Tanesco wamesema.
 
Mfufue magufuri aje akupe umeme usio katika mana unanongwa. Hata gari tu wanafanya matengenezo.
😃😃😃😃 Hawa wamlaumu Mwendazake alikuwa busy na Bwawa la umeme ila hakufanya matengenezo ya mitambo.

Pia Ali enjoy drop of economy so haikuleta shida.
 
Sasa hapo umetoka kwenye hoja umeanza matusi. Matusi nayajua sana,ila mimi sio kama wewe, najiheshimu. Napenda ninachokiweka humu mwingine akikipitia apate kitu. Ukishindwa hoja usilamishe wakuamini unachotaka kwa matusi.
Usiangalie kipengele kimoja,hoja zipi humo hujaona?
 
Anaongea kama vile anasema na familia yake hajui tumemwajiri kwa mda tu
 
Matengenezo ya kila siku toka uingie kwenye hiyo nafasi?. Ndio matengenezo gani hayo?. Hata kipindi cha Magu matengenezo yalikuwepo. Lakini sio kama hayo yenu
Sio tuu ya kila siku bali yanahitaji til.4.

Unataka tukuteue wewe umeme utaacha kukatika?
 
Makamba!Makamba!Makamba,naunga mkono juhudi zote hizo za kurekebisha miundombinu na ndiyo italeta tija.

Suala la kujenga chuo Mtwara fikirieni upya,Kwa aliyewahi kufika Lindi atakubaliana nami kuwa mkoa huo umedidimia kiuchumi kwakuwa kila kitu kitakachokusanya watu wengi ambazo ndiyo shughuli za kuboost uchumi kimepelekwa Mtwara na kuufanya mkoa wa Lindi kuwa hoi.

CHUO JENGENI LINDI angalau itahakikisha kuwa na idadi fulani ya watu wanaolipwa kuishi hapo kwa muda wote na kuboost uchumi wake,hata kuwepo kwa wanafunzi pia maana wengi watakopeshwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…