Waziri Makamba waelekeze Tanesco waache kusambaza umeme kwa nyaya nyembamba za 25mm badala ya 100mm wanaua vifaa vyetu

Waziri Makamba waelekeze Tanesco waache kusambaza umeme kwa nyaya nyembamba za 25mm badala ya 100mm wanaua vifaa vyetu

sasa mkuu ndiyo wapitishe 100mm kweli ?
napinga uliposema 'maeneo mengi sana' yanasambazwa na 25mm kitu ambacho siyo kweli
huo ni upotoshaji
Acha tu Mkuu Leo tumekutana na Wataalam wa umeme
Nijuavyo majumbani wire wa 6mm au 10 ndio unatumika kutoka kwenye mita kuingia ndani ya nyumba, halafu vijijini umeme wa REA hauhitaji transformer kila mita 1000 inaweza tosha Kijiji kimoja transformer moja
 
Unaijua 100mm vizuri kuwa serious kaka, na Mara nyingi TANESCO wanatumia 95mm na sio 100mm
Nakuhurumia kubishana na mimi,nime experience hii kitu kwa muda mrefu ikanitia hasara pia,kutokana na hilo nilipata wasaha wakufuatilia kwa kina,data ninazotoa hapa pata muda fuatilia Tanesco situngi ila ndivyo ilivyo 100mm ndio standard inayotakiwa kwenye distribution line,tanesco wanatumia terminology wanaita (point five) wakimaanisha waya wa 100mm
 
Acha tu Mkuu Leo tumekutana na Wataalam wa umeme
Nijuavyo majumbani wire wa 6mm au 10 ndio unatumika kutoka kwenye mita kuingia ndani ya nyumba, halafu vijijini umeme wa REA hauhitaji transformer kila mita 1000 inaweza tosha Kijiji kimoja transformer moja
Tatizo hujui,transformer inatakiwa kusambaza umeme kwa diameter ya kilomita moja (1000m) kila upande kuelekea kwa mteja,hii sio siasa ni technical demand.Kwa mteja yeyote atakaekuwa umbali wa zaidi ya 1000m kutoka kwenye transformer atambue kutakuwa na voltage drop yaani umeme unaanza kupoteza nguvu.Haya ni mambo yakitaalam sio ngonjera.Mpaka hapo wewe ni mweupe jaribu kuuliza upate faida.
Ninyi ndio baadhi yenu mnaajiriwa Tanesco kwa migongo ya wajomba zenu halafu mnaanza kututesa.
 
Ndugu upo sahihi sema naogopa kuitwa mweupe kichwan na mtoa mada

Ila kwa issue ya wire mm100 kubwa sana nadhani analenga Kutoka mtera au kidatu kwenda kwa mteja

Ukubwa wa transformer pia unatofautiana mita 1000 anaposema zitapoteza nguvu ni mwongo tu inategemea na matumiz /kiwango cha hao waliopo ndani ya hizo m 1000 na pia ukubwa wa transifoma
 
Nakuhurumia kubishana na mimi,nime experience hii kitu kwa muda mrefu ikanitia hasara pia,kutokana na hilo nilipata wasaha wakufuatilia kwa kina,data ninazotoa hapa pata muda fuatilia Tanesco situngi ila ndivyo ilivyo 100mm ndio standard inayotakiwa kwenye distribution line,tanesco wanatumia terminology wanaita (point five) wakimaanisha waya wa 100mm
Nishafanya kazi kwenye kiwanda Cha cable na kampuni ya electric yenye tender za REA nauhakika na ninachoongea mim ndo nakuonea huruma kwa sababu hujui kitu waya size kubwa ni 95mm ambayo ni size, na TANESCO na kampuni husika lazma waifanyie FIT kabla hawajaichukua hivi vitu vinaenda kitaalamu

2.5mm zinakua kwenye bobbin 16 alafu zinafanyiwa stranding ndo wanapata 95mm hiyo mostly ndo size ya kubwa kwa watu wa majumbani hio 100mm ni ya kwako
 
Hili ni kweli kabisa ,mimi ninaexperience hili tatizo la low voltage ,nyumba ni mpya, taa hua kuna mda zinazima kabisa ,fridge ndio likawa haliwaki,mana hua nina fridge guard hivyo kila mda fridge linajizima tu sababu umeme hauko sawa,sasa baada ya kusumbuana nao sana hatimae wakanitembelea na wakanifundisha kucheki voltage kwenye kiremote cha kuwekea umeme, zikawa ndogo zinakuja 150 na hazitulii zinapanda na kushuka kusababisha umeme kucheza kila mda,wakatengeneza hapo uongo na kweli angalau sasa hivi sio sana ila bado tatizo ninalo hata fridge sahivi imebidi niache kuliwasha kuna viashiria limeanza kuharibika ,asante mtoa mada sasa nimeelewa shida ilipo
 
Makamba is a failure minister anabebwa tu connection ya baba yake
 
Tatizo hujui,transformer inatakiwa kusambaza umeme kwa diameter ya kilomita moja (1000m) kila upande kuelekea kwa mteja,hii sio siasa ni technical demand.Kwa mteja yeyote atakaekuwa umbali wa zaidi ya 1000m kutoka kwenye transformer atambue kutakuwa na voltage drop yaani umeme unaanza kupoteza nguvu.Haya ni mambo yakitaalam sio ngonjera.Mpaka hapo wewe ni mweupe jaribu kuuliza upate faida.
Ninyi ndio baadhi yenu mnaajiriwa Tanesco kwa migongo ya wajomba zenu halafu mnaanza kututesa.
wewe ni muongo na mweupe kwa huo umeme, huku mjini Transfomer zinaweza kuwekwa hata mitaa 2 tu wakaweka nyingine Mfano kwenye maofisi, Hospital nk tofauti na umeme wa Vijijini (REA)
ni maajabu eti umeme ukisafiri Kilometa moja unakosa nguvu
humo njiani kutoka Mtera kwenda Mwanza kupitia na migodi si ungefia mfu (sio Live)
Transfomer Step down zinapokea nyanya 3 za 11KV na inaupunguza kutoka 33KV hadi matumizi yetu ya 240 v au ninyi wenye mashine za kusaga mnapewa mahitaji yenu kn ni line 3 na earth lkn sio ukubwa wa 100m wire
huko vijijini wanasaga pia kwa umeme wa REA
 
Back
Top Bottom