Waziri Mambo ya Nje ya nchi Dr Balozi Kombo tolea ufafanuzi kukatwa Msaada ya TB, Malaria na UKIMWI kwa Tanzania

Waziri Mambo ya Nje ya nchi Dr Balozi Kombo tolea ufafanuzi kukatwa Msaada ya TB, Malaria na UKIMWI kwa Tanzania

M24 Headquarters-Kigali

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2012
Posts
8,199
Reaction score
8,186
Mheshimiwa huu ni wakati wa wewe kuitisha Mkutano na kufafanua mambo ya Kimataifa ikiwamo usitishwaji wa Msaada kwa Tanzania. Nataarifiwa EU nao wapo mbioni.
 
Mambo kama haya yanayohusu uhai wa watu serikali ni wazito sana kutoka hadharani kutoa ufafanuzi.. hata machawa kina Lucas huwezi wasikia..halafu wanadai waendelee kuongoza..
 
Attachments

Mheshimiwa huu ni wakati wa wewe kuitisha Mkutano na kufafanua mambo ya Kimataifa ikiwamo usitishwaji wa Msaada kwa Tanzania. Nataarifiwa EU nao wapo mbioni.
Ni kweli,
swala ni kwamba tukifa tutatoa awamu nyingine ya kizazi, vinginevyo ni kueneza maambukizi.
Hata Chalamila juzi alisema ukweli sema ujumbe wake haukufika vizuri.
Unaendaje kupata mimba, halafu unakosa elfu 50 kuwapa madaktari wakuzalishe.
 
Ajira zote kupitia USAID zimekufa rasmi

Dawa zitaendelea kutolewa Kwa miezi 6 Baada ya hapo Kila nchi ijitegemee
Kitendo cha kusema dawa zimesitishwa tayari uhaba utakuwepo kuanzia sasa maana wajanja wachache watazificha ili kupiga hela na baadhi ya waathirika wenye uwezo watanunua nyingi na kusababisha uhaba!
 
Kuna wakati NGO zinazojihusisha na masuala ya afya na uzazi wa mpango hasa zinazofadhiliwa na US zilikuwa zikiandamwa kwa “kuhamasisha ushoga” nchini.

Na kweli misaada ya kupambana na ukimwi haikosi kipengele cha focus on lgbt community.

Nilidhani kusitishwa kwa misaada ya US kutapokelewa vyema na wanaochukia mabeberu kwa “kulazimisha” ushoga nchini. Au ndio imekuwa tena hadithi ya baniani mbaya …
 
Bado nasubiri waje wakiunga mkono hatua ya kusitishwa kwa misaada toka Marekani.
 
Vipi miradi mikubwa ya malaria nchini kama ile ya ifakara na Bagamoyo, utapona kweli?
 
Amelegeza masharti kwenye upande wa hizo dawa.
Vijana endeleeni kutembelea rimu tu. Dawa zitaendelea kuja
 
Bado nasubiri waje wakiunga mkono hatua ya kusitishwa kwa misaada toka Marekani.
Utachoka bure. Watanzania wengi hawana uwezo au hulka ya kuunganisha mambo kichwani.

Nimezungukwa na jamaa wasiotaka kabisa kusikia habari ya demokrasia na haki za binadamu kwa vile tu vimewekwa vipengele vya lgbt. Hivyo Azimio lote la haki za binadamu halina maana.

Trump amesitisha misaada hiyo kwa vile ameahidi base yake (wapiga kura wake) kufuta misaada yote inayohusiana na lgbt. Kasingizia anaichambua ili kuhakikisha misaada hiyo haiendi kuimarisha itikadi “zilizopinda”! Anastahili kuungwa mkono wa dhati na wote “wanaopinga ushoga”. Period. Usipokubaliana na Trump, jipime mwenyewe umesimama wapi.
 
Back
Top Bottom