Waziri Masauni akabidhi magari 77 kwa Jeshi la Polisi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amelikabidhi Jeshi la Polisi magari 77 kwa ajili kurahisha utekelezaji wa majukumu yake ya kusimamia usalama wa raia na mali zao ikiwa ni mwendelezo jitihada za Serikali kulifanya Jeshi hilo kuwa la kisasa lenye vifaa, na weledi wa kuzuia uhalifu.

Akikabidhi magari hayo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Waziri Masauni amelitaka Jeshi hilo kuhakikisha kuwa linayatumia vyema magari hayo kwa kupunguza malalamiko ya wananchi dhidi ya Jeshi la Polisi ikiwa ni sambamba na kuyatunza ili kuthamini jitihada za Serikali kuliboresha Jeshi hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP. Camillus Wambura ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi hilo kuwa la kisasa hivyo ni wajibu Polisi kuhakikisha uhalifu unaendelea kupungua huku akiwaasa madereva wa magari hayo kuzingatia sheria za usalama barabarani ili magari hayo yaweze kudumu.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama, Mhe. Vita Kawawa ametoa rai kwa madereva wa magari hayo kupatiwa mafunzo huku Mkurugenzi wa Kampuni ya Kifaru Motors, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo akiahidi kuwa kampuni yake imejiandaa kulisaidia Jeshi hilo msaada kitaalamu, ushauri na kiufundi pale itakapohitajika.
WhatsApp Image 2024-10-19 at 15.59.17_a1dd03cd.jpg

WhatsApp Image 2024-10-19 at 15.59.17_a6064fbe.jpg

WhatsApp Image 2024-10-19 at 15.59.19_7c2e0e3e.jpg

WhatsApp Image 2024-10-19 at 15.59.18_836e2025.jpg

WhatsApp Image 2024-10-19 at 15.59.19_99d02fe5.jpg
 
Vijana sio kama nawabeza ila wazeni zaidi kujiajiri nishaona hakuna mpango wa kueleweka kupunguza jobless kitaa..kama wewe ni msomi tafuta tu kitu cha kufanya..kipaumbele nishakijua za serikali YETU
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amelikabidhi Jeshi la Polisi magari 77 kwa ajili kurahisha utekelezaji wa majukumu yake ya kusimamia usalama wa raia na mali zao ikiwa ni mwendelezo jitihada za Serikali kulifanya Jeshi hilo kuwa la kisasa lenye vifaa, na weledi wa kuzuia uhalifu.

Akikabidhi magari hayo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Waziri Masauni amelitaka Jeshi hilo kuhakikisha kuwa linayatumia vyema magari hayo kwa kupunguza malalamiko ya wananchi dhidi ya Jeshi la Polisi ikiwa ni sambamba na kuyatunza ili kuthamini jitihada za Serikali kuliboresha Jeshi hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP. Camillus Wambura ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi hilo kuwa la kisasa hivyo ni wajibu Polisi kuhakikisha uhalifu unaendelea kupungua huku akiwaasa madereva wa magari hayo kuzingatia sheria za usalama barabarani ili magari hayo yaweze kudumu.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama, Mhe. Vita Kawawa ametoa rai kwa madereva wa magari hayo kupatiwa mafunzo huku Mkurugenzi wa Kampuni ya Kifaru Motors, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo akiahidi kuwa kampuni yake imejiandaa kulisaidia Jeshi hilo msaada kitaalamu, ushauri na kiufundi pale itakapohitajika.
Chadema watasema ni ma V8 yanaliza pesa 😂😂
 
Jeshi la magari ndo jeshi gani tena? Ina maana kuna jeshi jingine limeundwa?
 
Hizo gari ni wazi zinaenda kwenye administration kwa maana kubeba viongozi nk haziendi kumgusa mwananchi moja kwa moja. Wananchi wanataka uonevu uishe tu
 
Yana mwisho

Ninamkumbuka IGP Harun Mahundi na uadilifu wake utarudi. Nilikuwa nakua. Ila hakukuwa na mbambamba. Baada yake sasa 😂 😂 😂 😂 😂

Inaelekea siasa za vyama vingi zimeleta changamoto ambazo pengine kitaalamu hazijasomwa na kujua namna ya kuzipatia ufumbuzi
 
Hata safety parking ya hayo magari hakuna,
Njooni 2025, muje muangalie walivyo kingoroka
 
Ofisi na nyumba za polisi ndio zinaongoza kwa uchakavu. Mtu analala nyumba ya 1980's haijafanyiwa ukarabati hawezi tunza gari
 
Wanaa wamepewa magari sasa ndugu zangu wapinzani tukitea tea tunakula vya kutosha
 
Ma afisa nao huwa wanafanya doria mbona gar za kutembelea ma afisa na sio za doria
 
Back
Top Bottom