Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (kushoto) baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi ambayo inahusu masuala yanayohusu Wakimbizi waliopo katika makambi yanayopatikana mkoani humo.
Wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Sudi Mwakibasi na Mkurugenzi Msaidizi wa Usimamizi wa Kambi na Makazi, Kamishna wa Polisi, Mohammed Hassan.