JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Waziri Masauni ameyasema hayo tarehe 29 Septemba, 2024 alipotembelea na kuzungumza na Maafisa wa Gereza la Kilimo na Mifugo Kitai, Mbinga Mkoani Ruvuma ambapo amesema miongoni mwa maboresho hayo ni kutenganisha mamlaka ya kiutawala ya Jeshi la Magereza na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi hilo (SHIMA), ambapo maboresho yatakwenda kuleta ufanisi wa usimamizi wa mauasala ya kiutawala na biashara.
Aidha, Waziri Masauni katika hatua nyingine ametoa maagizo kwa magereza ya uzalishaji mali nchini nzima kuchangamkia fursa za kilimo cha mazao ya nafaka kwa kutanua maeneo ya mashamba ili kuendana na jitihada za Serikali katika kuinua sekta ya kilimo.
Sambamba na hilo Mhandisi Masauni alisisitiza matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuacha na matumizi ya kuni na mkaa katika magereza ili kuendana na ajenda ya Afrika na Dunia katika kutunza mazingira.
Kwa upande wake Mkuu wa Gereza la Kilimo na Mifugo Kitai SP. Gabriel Luderi amesema Gereza hilo lipo tayari kupokea na kuendana na mabadiliko yakatayoongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na kuboresha utendaji kazi wa Jeshi la Magereza.
Awali, Waziri Masauni alitembelea Gereza hilo Mwaka 2019 akiwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo ambapo amesema licha ya kuwa sasa kuna mabadiliko lakini alitarajia kuona mabadiliko makubwa zaidi ya Kilimo katika gereza hilo.
CHANZO: Wizara ya Ndani