Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amelazimika kutoka Ofisini na kufuatilia utendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambapo mamlaka hiyo imekuwa ikilalamikiwa na Wananchi kwa utendaji na utoaji wa Vitambulisho usioridhisha.
Waziri Masauni amefika katika Ofisi ya NIDA iliyopo Manispaa ya Ubungo na kukuta zaidi ya Wananchi 100 wakiwemo Wanafunzi waliohitimu Kidato cha Sita, hivi karibuni waliopo katika mchakato wa kuomba mkopo wa Elimu ya Juu wanatakiwa kuwa na Kitambulisho cha Taifa wakiwa hawapati huduma wanayostahili.
Pia soma;
KERO - Ugawaji wa NIDA wilaya ya Busega unasuasua zaidi ya mwezi. Wanafunzi tunaotegemea namba kuomba mkopo HESLB hatarini kukwama